Dollar

38,5992

0.33 %

Euro

43,6545

0.2 %

Gram Gold

4.017,2800

0.33 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Tume ya kitaifa ya haki za binadamu nchini Sudan imeshtumu ‘ukiukwaji mkubwa uliotekelezwa na vikosi vya RSF dhidi ya raia huko Al-Nahud’

Idadi ya waliouawa katika shambulizi la Al-Nahud Sudan yafika 300: Tume ya haki

Tume ya kitaifa ya kutetea haki za binadamu ya Sudan siku ya Jumamosi imetangaza kuwa raia wasiopungua 300, ikiwemo watoto 21 na wanawake 15, waliuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi la RSF katika mji wa Al-Nahud kwenye jimbo la Kordofan Magharibi.

Katika taarifa rasmi, tume hiyo imeshtumu hilo kuwa “ukiukwaji mkubwa uliotekelezwa na kundi la RSF dhidi ya raia wa Al-Nahud, ikiwemo kuwalenga kwa makusudi, kuwapiga risasi kwa karibu, na kuwaua.”

Tume ilisema kuwa idadi hiyo ya vifo ni ya muda tu kwa sasa kwa sababu bado mashambulizi yanaendelea katika mji huo kwa sababu wapiganaji wa RSF wanazuia misaada na kutoruhusu watu kuondoka eneo hilo.

Siku ya Ijumaa, Shirika la mtandao wa Madaktari Sudan lilisema kuwa watu zaidi ya 100 wameuawa kwenye shambulizi hilo.

Kulingana na tume hiyo, RSF pia ilipora dawa, bidhaa sokoni, na katika hospitali ya Al-Nahud.

Ilitoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuweka shinikizo kwa pande zote mbili kuhakikisha kuwa raia wanaruhusiwa kupitia njia salama mbali na maeneo ya mapigano.

Hakujakuwa na taarifa yoyote kutoka kwa kundi la RSF.

Siku ya Ijumaa RSF ilidai kuwa imechukua udhibiti kamili wa Al-Nahud na kuingia ndani ya makao makuu ya kitengo cha 18 cha jeshi la Sudan baada ya makabiliano na vikosi vya serikali.

Mji huo, ambao zamani ulikuwa kwenye udhibiti wa jeshi, umekuwa makao makuu ya muda ya jimbo la Kordofan Magharibi tangu Julai 2024, baada ya RSF kuchukua udhibiti wa makao makuu yake halisi, mji wa Al-Fula.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#