Sport
Dollar
38,5992
0.33 %Euro
43,6545
0.2 %Gram Gold
4.017,2800
0.33 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Brice Oligui Nguema alishinda uchaguzi wa mwezi uliopita akipata asilimia 95 ya kura baada ya kuongoza serikali ya mpito kwa miezi 19.
Rais mteule wa Gabon Brice Oligui Nguema ambaye aliongoza mapinduzi yaliyomaliza utawala wa miongo kadhaa wa familia ya Bongo na kushinda kwa kishindo mwezi uliopita akipata asilimia 95 ya kura ataapishwa siku ya Jumamosi.
Jenerali huyo, alimpindua Ali Bongo mwezi Agosti 2023 na kumaliza utawala wa miaka 55 wa familia ya Bongo, anachukua wadhifa wa urais rasmi baada ya kuongoza serikali ya mpito kwa miezi 19.
Viongozi mbalimbali kutoka bara la Afrika wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo katika uwanja wenye uwezo wa kuingia watu 40,000, kaskazini mwa mji wa Libreville.
Miongoni mwao ni Adama Barrow wa Gambia, Bassirou Diomaye Faye wa Senegal,Ismail Omar Guelleh wa Djibouti na Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa Guinea ya Ikweta.
Uwanja
Kulingana na vyombo vya habari vya ndani na kimataifa, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi pia anatarajiwa, pamoja na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame, ambaye kuhudhuria kwake kulithibitishwa na wizara ya mambo ya nje ya Rwanda.
DRC na Rwanda kwa sasa hivi wako kwenye mazungumzo ya kumaliza mapigano mashariki mwa Congo.
Tiketi za kuhudhuria hafla hiyo katika uwanja wa Angondje ziiligawanywa bila malipo, kwa uga huo uliojengwa kutokana na urafiki kati ya Gabon na China, na itakuwa mara ya kwanza kwa nchi hiyo kufanya sherehe ya kuapishwa kwa rais hadharani.
Kulingana na shirika la habari la taifa, kutakuwa na wasanii watakaotoa burudani pamoja na gwaride la wanajeshi, na baadaye kutakuwa na "tamasha la ushindi" litakalofanyika katika sehemu ya bahari ya Libreville jioni.
Umma umeshirikishwa
Kwa wiki kadhaa, mamia ya wafanyakazi wamekuwa wakisafisha na kupaka rangi maeneo ya barabara kuu zinazoelekea katika uwanja huo.
Mamlaka na chombo cha habari cha serikali wametaka watu kuonesha uzalendo wakati wageni kutoka nje watakapokuja nchini kwao.
"Raia wote wa jiji la Libreville wanaombwa kuwapokea vizuri wageni wetu wa heshima," wizara ya mambo ya ndani ilisema katika taarifa.
Iliwataka wale wanaoishi karibu na uwanja huo "kushiriki katika kusafisha na kupamba" maeneo yao.
Changamoto kubwa
Oligui, 50, anakabiliwa na changamoto kubwa katika kuongoza taifa hilo lenye utajiri wa mafuta, akihitajika kuimarisha miundombinu muhimu na kuangazia maeneo mengine ya uwekezaji katika kukuza uchumi wakati nchi ikiwa na deni kubwa.
Miongoni mwa masuala yanayohitaji kushughulikiwa ni mifumo ya umeme ambayo ni ya zamani sana na mara nyingi umeme unakatika, ukosefu wa ajira kwa vijana ambao umefikia asilimia 40, barabara mbovu au sehemu nyingine hakuna barabara kabisa na deni linaloongezeka.
Wakati wa kipindi cha mpito, Oligui alijieleza yeye kama "mjenzi", akizindua miradi mbalimbali ya ujenzi, huku akiapa "kukabiliana" na ufisadi na kuirejesha nchi katika hali nzuri.
Comments
No comments Yet
Comment