Sport
Rais Cyril Ramaphosa ameutaja uhalifu wa magenge kuwa tishio kwa maendeleo ya demokrasia na uchumi nchini Afrika Kusini.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza siku ya Alhamisi kuwa ataagiza jeshi lifanye kazi kwa karibu na polisi kukabiliana na viwango vikubwa vya uhalifu wa magenge.
Viwango vikubwa vya mauaji nchini humo karibu watu 60 wanauawa kila siku ikiwemo yale ya vita kati ya magenge ya dawa za kulevya mjini Cape Town na ufyatulianaji risasi unaohusishwa na uchimbaji haramu wa madini jijini Johannesburg mkoa wa Gauteng.
"Uhalifu wa magenge sasa hivi ndiyo tishio kubwa kwa maendeleo yetu ya demokrasia, jamii na ya kiuchumi," Ramaphosa alisema katika hotuba yake ya kila mwaka kwa taifa.
"Nitaagiza jesho la Afrika Kusini kwenda kusaidia polisi," aliyaambia mabunge yote mawili ya Afrika Kusini .
Andaeni mpangokazi
Ramaphosa ameagiza wakuu wa polisi na jeshi kuandaa mpangokazi ambapo "vikosi vyetu vya usalama viende huko katika siku chache zijazo Western Cape na Gauteng kukabiliana na magenge ya uhalifu na uchimbaji haramu wa madini."
Hatua zingine za kukabiliana na uhalifu ni kuajiri maafisa 5,500 wa polisi na kuimarisha ukusanyaji taarifa za kijasusi wakati wakilipa kipaumbele suala la kutambua makundi ya uhalifu, alisema.
"Kukithiri kwa uhalifu kunapimwa kutokana na watu kupoteza maisha na mustakabali wa watu kukatizwa. Unapimwa pia kutokana na hofu inayoingia katika jamii yetu na kusitasita kwa uwekezaji katika biashara," Ramaphosa alisema.
Comments
No comments Yet
Comment