Dkt. Akwilapo amesema mwenendo wa kuhodhi maeneo bila ya kuyaendeleza unakwamisha mipango ya maendeleo ya miji na matumizi bora ya ardhi.

Wasioendeleza ardhi kwa miaka mitatu Tanzania kunyang'anywa na serikali

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  nchini Tanzania Dkt Leonard Akwilapo, amewataka Watanzania wanaohodhi maeneo kuhakikisha wanayaendeleza ndani ya muda wa kisheria, ambao ni miaka mitatu.

Dkt. Akwilapo amesema mwenendo wa kuhodhi maeneo bila ya kuyaendeleza unakwamisha mipango ya maendeleo ya miji na matumizi bora ya ardhi.

"Bado natafakari nini cha kufanya maana sheria ipo. Usipoendeleza eneo lako ndani ya miaka mitatu unaweza kunyang'anywa," amesema hayo Waziri Akwilapo alipokuwa jijini Arusha Februari 11 katika ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba  la Taifa.

Kwa mujibu wa sheria ya Ardhi nchini Tanzania, Sura ya 113, kifungu cha 49, mmiliki wa ardhi anatakiwa kuendeleza eneo lake ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya kupata umiliki, vinginevyo serikali ina mamlaka ya kulichukua endapo sharti hilo halitazingatiwa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#