Wakati huohuo, Waziri Mkuu huyo wa Tanzania, ameitaka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania na Vyombo vya ulinzi kuhakikisha hakuna bidhaa za magendo zinazoingia nchini.

Waziri Mkuu wa Tanzania Mwigulu Nchemba ataka mikakati ya kulinda viwanda vya ndani

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba amezitaka Taasisi za udhibiti za Serikali kuweka kipaumbele katika kulinda viwanda vya ndani na biashara badala ya kuwa kikwazo katika kufikia mafanikio.

Mwigulu amesema kuwa haitakuwa rahisi kulinda viwanda na biashara za ndani kama Tanzania itakuwa jalala la bidhaa kutoka nje.

“Wizara ya fedha hakikisheni hamtoi msamaha wala unafuu wa kodi katika bidhaa za nje ambazo zinapatikana ndani ya nchi. Toeni unafuu wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi kama uzalishaji ndani ya nchi hatujitoshelezi,” alisema Mwigulu wakati akizindua kiwanda cha mabati cha Lodhia kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu huyo wa Tanzania, ameitaka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania na Vyombo vya ulinzi kuhakikisha hakuna bidhaa za  magendo zinazoingia nchini.

“Taasisi zote na vyombo vya ulinzi simamieni uingizaji wa bidhaa ndani na ufuate utaratibu, msipofanya hivyo mtaua uwekezaji unaofanywa ndani,” alielekeza.

Kulingana na Mwigulu, sekta binafsi ni mdau mkubwa katika maendeleo na injini ya kuchachusha utekelezaji wa miradi.

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara  nchini humo Judith Kapinga, alisema kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuchukua hatua za makusudi za kulinda viwanda vya ndani na kuweka mazingira mazuri ya kuongezeka vingine.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#