Sport
Barre amepongeza mpango huo wa uchimbaji na Uturuki kama chachu ya ukuaji wa Somalia
Waziri Mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre siku ya Jumatatu amepongeza kuanzishwa kwa uchimbaji mafuta baharini na Uturuki katika pwani ya Somalia kama hatua ya “kihistoria”, huku meli ya Uturuki ya uchimbaji mafuta ya Cagri Bey ikielekea kwa majukumu yake ya kwanza nje ya nchi.
“Leo, kwa Cagri Bey, tunaona tunaweza kushuhudia mwanzo wa jambo kubwa — ukurasa mpya wa mabadiliko ya kweli kiuchumi,” Barre aliandika kwenye mtandao wa X.
Alieleza hatua hiyo kama wakati ambao utajiri asili wa Somalia unapoanza kutoa uwezo kwa taifa na kuwa na matokeo ya msingi kwa watu.
“Vizazi na vizazi vya watu wetu vimekuwa vikiskia Somalia ina utajiri wa rasilimali; lakini kwa miongo kadhaa wamesubiri ahadi itimie. Sasa hakuna tena kusubiri. Mambo mazuri yametufikia,” Barre alisema.
Alipongeza “Undugu wa Uturuki,” na Somalia unaoongozwa na Rais Recep Tayyip Erdogan, kwa kuchagua kama sehemu ya kwanza ya mradi wa kihistoria.
“Uamuzi huu ni zaidi wa kimkakati — ni ishara ya imani inayovuka mipaka na ushahidi wa ushirikiano unaokuwa kati ya Uturuki na Somalia, wenye mizizi yake katika undugu na matumaini ya kuwa na mustakabali mzuri,” aliongeza.
Cagri Bey, ambayo iliondoka bandari ya kusini ya Tasucu katika mkoa wa Mersin siku ya Jumapili, inatarajiwa kufika Mogadishu katika kipindi cha siku 45 na kuanza uchimbaji mwezi Aprili katika kisima cha Curad-1.
Uturuki na Somalia walitia saini makubaliano 2024 ya kuchimba mafuta ndani na nje ya bahari na gesi. Meli kubwa ya Oruc Reis awali ilikamilisha kufanya tathmini katika maeneo matatu ya mafuta.
Comments
No comments Yet
Comment