Dollar

39,1011

0.04 %

Euro

44,4609

0.52 %

Gram Gold

4.202,2600

1.92 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kitengo cha makosa ya jinai nchini Kenya kimesema uchunguzi umebaini kuwa watatu hao kutoka Uganda waliwasili nchini Kenya tarehe Mei 21, 2025 kupitia mpaka wa Malaba.

Washukiwa watatu wa wizi kutoka Uganda wakamatwa Kenya

Washukiwa wanne wa ujambazi wakiwemo raia watatu wa Uganda na Mkenya mmoja wamekamatwa na bunduki tatu mjini Nairobi.

Polisi ya Kenya imesema kukamatwa kwao kulifuatia msako uliofanywa katika maeneo ya Dandora, Saika, Pumwani na Huruma, jijini humo.

Msako huo ulifanywa Alhamisi, Mei 22 ulifuatia ripoti za wizi wa kutumia silaha ulioripotiwa kufanywa na genge katika maeneo ya Nairobi.

Timu ya kitengo cha makosa ya jinai, DCI ikiungwa mkono na wenzao katika Ofisi ya Ujasusi ilianzisha msako kwa kila mmoja wa washukiwa wanne, na kufanikiwa kuwapata wote na bastola mbili, bunduki aina ya AK 47 na risasi 50.

Washukiwa hao walitambuliwa kama Sipholi Sam Wafula almaarufu Sande, Ogomba Alex, Mohammed Musa na Wafula Clinton.

“Sipholi ndiye aliyekuwa wa kwanza kukanyaga nyavu za polisi, ambaye katika mahojiano aliwaongoza askari hao hadi kwenye nyumba yake ya kupanga ambako bastola aina ya Falcon iliyokuwa na risasi kumi na moja (11) iligunduliwa chini ya mto,” Polisi imeelezea katika taarifa mtandaoni.

“Vile vile, Ogomba Alex alishikwa katika nyumba yake ya kupanga iliyopo Dandora ambapo alipatikana na bunduki ya kivita aina ya AK47 iliyokuwa na risasi thelathini (30) ambayo ilikuwa imefichwa chini ya kochi lake,” Polisi imeongezea.

Kuhojiwa kwa muda mfupi kwa washukiwa hao wawili kuliongoza wapelelezi hadi nyumbani kwa Mohammed Musa katika eneo linaloitwa Huruma ambako amekuwa akiishi na familia yake. Imethibitishwa kuwa yeye ndiye mmiliki wa bunduki ya AK47.

“Uchunguzi wa awali hadi sasa umebaini kuwa watatu hao wa Uganda waliwasili nchini Kenya tarehe Mei 21, 2025 kupitia mpaka wa Malaba, baada ya kutoweka katika nchi jirani.”

Wafula Clinton (Mkenya), 45, mkaazi wa Githurai na anayedaiwa kuwa kiongozi wa genge hilo, alikamatwa katika eneo la Pumwani.

Inadaiwa amehusika mara kwa mara katika uhalifu. Wakati wa kukamatwa na kupekuliwa, Polisi inasema ilipata bastola ya pili, Palleberum Feg .9mm iliyokuwa na risasi tisa ilipatikana imewekwa kiunoni.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#