Dollar

39,1011

0.04 %

Euro

44,4609

0.52 %

Gram Gold

4.202,2600

1.92 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Joseph Kabila ambaye aliiongoza DRC kuanzia 2001 hadi 2019, sasa anakabiliwa na uwezekano wa kufikishwa katika mahakama za kijeshi kwa tuhuma za "uhaini, uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu na kushiriki katika harakati za uasi."

DRC yamuondolea kinga rais mstaafu Joseph Kabila

Bunge la Seneti la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC siku ya Alhamisi lilipiga kura ya kumuondolea kinga aliyekuwa rais wa nchi hiyo Joseph Kabila.

DRC inamtuhumu kiongozi huyo wa zamani kwa kuunga mkono wanamgambo wa M23 katika eneo la mashariki lenye utajiri wa madini.

Kwa kura 88 kwa watano, Baraza la Juu la Bunge liliunga mkono kumuweka kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 53 mbele ya mashtaka kwa tuhuma za kuunga mkono kundi la waasi la M23, ambalo limeteka maeneo mengi ya mashariki mwa DRC kwa msaada wa Rwanda. Rwanda imeendelea kuzikana tuhuma hizo.

Mrithi wake, Rais Felix Tshisekedi, anamshutumu Kabila kwa kula njama na M23, ambao mashambulizi yao ya hivi majuzi yamezidisha mzozo wa mashariki wa zaidi ya miongo mitatu.

Kabila, ambaye amekuwa nje ya nchi tangu 2023, hakuwepo katika ukumbi wa Bunge wakati wa upigaji kura, huku wajumbe wake wakishindwa.

Kwa kura hiyo, "Seneti inaidhinisha kufunguliwa mashtaka na kuondolewa kwa kinga ya Joseph Kabila," alisema Spika wa Baraza la Juu Jean-Michel Sama Lukonde.

Kabila hivi sasa, 2019, sasa anakabiliwa na uwezekano wa kufikishwa katika mahakama za kijeshi kwa "uhaini, uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na kushiriki katika harakati za uasi".

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#