Dollar

39,1011

0.04 %

Euro

44,4609

0.52 %

Gram Gold

4.202,2600

1.92 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inasema kuwa itaiwekea vikwazo serikali ya Sudan kwa madai ya kutumia silaha za kemikali katika vita vyao na wapiganaji wa RSF.

Marekani kuiwekea vikwazo Sudan kwa madai ya kutumia silaha za kemikali

Marekani imetangaza kuwa itaiwekea vikwazo Sudan baada ya ‘kuamua’ kuwa serikali hiyo ilitumia silaha za kemikali 2024 katika mapigano yake na vikosi vya paramilitary Rapid Support Forces (RSF).

Maamuzi hayo, ambayo yalibaini kuwa Sudan imeenda kinyume na makubaliano kuhusu matumizi ya silaha za kemikali (CWC), yaliwasilishwa siku ya Alhamisi, wizara ya mambo ya nje ilisema katika taarifa.

"Kufuatia kutoa taarifa katika kipindi cha siku 15 kwa bunge la Congress, Marekani itaiwekea vikwazo Sudan, ikiwemo vya kusafirisha bidhaa nchini Sudan na fursa ya mikopo ya serikali ya Marekani," ilisema.

Kuwepo kwa silaha za kemikali

"Marekani inatoa wito kwa serikali ya Sudan kuacha kutumia silaha za kemikali na kuzingatia jukumu lake chini ya makubaliano ya matumizi ya silaha hizo. Marekani imedhamiria kuwawajibisha wote wale waliohusika katika kusaidia kuwepo kwa silaha za kemikali," wizara hiyo ya Mambo ya Nje iliongeza.

Vikwazo hivyo vinatarajiwa kuanza kutekelezwa 6 Juni, baada ya kusajiliwa rasmi kwenye gazeti la serikali.

Hatua hizi za Marekani zinakuja huku jeshi la Sudan likipata mafanikio dhidi ya vikosi vya RSF, kuchukua udhibiti wa maeneo, ikiwemo mji mkuu Khartoum.

Tangu Aprili 2023, RSF imekuwa ikikabiliana na Jeshi la Sudan, mapigano yaliyosababisha mauaji ya maelfu ya watu na kuwepo kwa hali mbaya zaidi kwa watu duniani.

Kulingana na Umoja wa Mataifa na serikali za mitaa, watu zaidi ya 20,000 wameuawa na wengine milioni 15 kuondoka katika makazi yao.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#