Dollar

39,0313

0.28 %

Euro

44,3539

0.69 %

Gram Gold

4.220,7400

2.36 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kulingana na ripoti yake ni balozi 10 tu kati ya 38 zilizokaguliwa na kupokea ufadhili kutoka kwa serikali katika mwaka 2024.

Uganda kufunga baadhi ya balozi zake

Serikali ya Uganda sasa inafikiria kupunguza uwakilishi wake katika nchi za kigeni.

Hii inafuatia kuunganishwa kwa baadhi ya taasisi za serikali mwaka 2024.

“Rais aliiagiza wizara kuandaa ripoti ambayo itatumika kukamilisha mpango huo. Baada ya kukamilika, itapelekwa katika Baraza la Mawaziri ili kuhalalisha kufungwa kwa balozi yoyote,” Vincent Bagiire, ambae ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje aliiambia Kamati ya Bunge.

"Tuna agizo kutoka kwa Rais kufanya uchanganuzi wa faida ya gharama katika balozi 35 nje ya nchi kwa nia ya kuzipunguza hadi takriban 15. Kwa hivyo, wakati ajira bado ni changamoto, tunatazamia kupunguza idadi ya wafanyakazi,” Bagiire alisema.

Majadiliano hayo yaliibuka wakati wa kuzingatia ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa 2024 kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi.

Mkaguzi Mkuu alikuwa akielezea kuhusu kutokuwa na ufadhili wa kutosha katika bajeti za maendeleo ya mtaji kwa balozi kadhaa nje ya nchi.

Kulingana na ripoti yake ni balozi 10 tu kati ya 38 zilizokaguliwa na kupokea ufadhili kutoka kwa serikali katika mwaka 2024.

28 zilizosalia hazikupata fedha kwa ajili ya mahitaji ya dharura kama vile kubadilisha samani kuukuu, kununua vifaa vya TEHAMA, kununua magari ya matumizi na ukarabati wa makaazi ya balozi.

Ripoti iliyoletwa bungeni imeonyesha kuwa balozi za Uganda nje ya nchi zinahitaji zaidi ya dola milioni 109.

Hili ni ongezeko ya dola milioni 21 ya bajeti ya mwaka 2024/2025.

Uganda ina balozi 38 nje ya nchi huku ikiwa mwenyeji wa balozi 54 za kigeni.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#