Sport
Dollar
38,6044
0.09 %Euro
43,9386
0.54 %Gram Gold
4.239,9000
2.56 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Karibu maafisa 100 wa majeshi kutoka zaidi ya nchi 40, ikiwemo Misri, Msumbiji, Tanzania, na Kenya wanafanya ziara China hadi 15 Mei
Kulingana na taarifa rasmi, maafisa takriban 100 wa jeshi kutoka mataifa 40 ya Afrika wameanza ziara ya siku 10 nchini China kuanzia Jumatatu.
Maafisa hao kutoka mataifa ya Misri, Msumbiji, Tanzania, na Kenya, watakuwa ziarani nchini China hadi 15 Mei kwa hisani ya mualiko wa Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo.
Wakati wa ziara hiyo, ujumbe huo utashiriki katika majadiliano na China pamoja na kutembelea baadhi ya miji, ikiwemo Beijing, Changsha na Shaoshan katika mkoa wa Hunan ya kati, wizara imesema.
Mapema mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi aliahidi misaada ya kijeshi kwa Afrika yenye thamani ya yuan bilioni 1 (sawa na dola milioni 136 ) wakati wa ziara yake nchini Namibia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Chad, na Nigeria.
Wang pia amesema China itasaidia kuwapa mafunzo wanajeshi 6,000 na polisi 1,000 kote barani Afrika.
Ziara hii ya wajumbe kutoka Afrika inafuata kumalizika kwa mafunzo ya pamoja kati ya China na Misri.
Mafunzo hayo ya siku 18, yaliyopewa jina la ‘Eagles of Civilization 2025’, yalifanyika katika kambi ya jeshi la anga la Misri na yalimalizika siku ya Jumapili.
Comments
No comments Yet
Comment