Sport
Dollar
38,6126
0.11 %Euro
43,8575
0.39 %Gram Gold
4.204,2500
1.7 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Mwaka 2024 Rais Ruto alishutumiwa na wananchi na wachambuzi wa kisiasa kwa kuchelewa kuunda Tume ya Uchaguzi.
Rais wa Kenya William Ruto amepokea ripoti ya watu waliopendekezwa kuajiriwa katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
“Nilipokea ripoti ya kuajiri walioteuliwa katika nyadhifa za Uenyekiti na Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutoka Jopo la Uchaguzi la IEBC, Ikulu ya Nairobi,” Rais Ruto alidhihirisha katika akaunti yake wa X.
Aidha alibainisha kuwa, atateua Makamishna na kupeleka majina yao Bungeni kwa ajili ya kuhakiki na kupitishwa, na baada ya hapo, uteuzi.
Mwaka 2024 Rais Ruto alilaumiwa na wananchi na wachambuzi wa kisiasa kwa kuchelewa kuunda Tume hiyo ya uchaguzi.
Januari 2025, akateua jopo la wataalamu 9 kufanya usaili wa vyeo tofauti vya IEBC,
“Nalipongeza jopo hilo linaloongozwa na Dkt. Nelson Makanda kwa kazi nzuri. Kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya IEBC, nitapendekeza na kuwasilisha majina hayo kwa Bunge la Kitaifa kwa kanuni za kikatiba zinazoongoza mfumo wetu wa uongozi,” alisema Rais Ruto.
Kukabidhiwa kwa ripoti hiyo kunafuatia kukamilika kwa usaili kwa mafanikio.
Jopo la uteuzi wa IEBC lilihitimisha usaili wake Aprili 25, kufuatia zoezi la uhakiki lililodumu kwa mwezi mzima.
Likiongozwa na Nelson Makanda, jopo hilo lilikamilisha mahojiano ya wadhifa wa mwenyekiti wa IEBC mnamo Machi 26.
Kati ya wagombea 111 walioteuliwa, 106 walifika mbele ya jopo kwa mahojiano.
Jumla ya wagombea 11 walihojiwa kwa nafasi ya mwenyekiti, akiwemo aliyekuwa Msajili Mkuu wa Mahakama Anne Amadi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utekelezaji Katiba Charles Nyachae.
Comments
No comments Yet
Comment