Sport
Dollar
38,6129
0.11 %Euro
43,9643
0.62 %Gram Gold
4.238,1200
2.51 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini yatoa hati za makosa kwa makampuni 95 ya uchimbaji madini yaliyokiuka masharti ya Leseni.
Serikali ya Tanzania imetoa Hati za Makosa kwa Kampuni 95 za Uchimbaji Mkubwa na wa Kati wa Madini kutokana na wamiliki wa leseni hizo kukiuka masharti ya Leseni kama yalivyoainishwa kwenye Sheria ya Madini.
Akizungumza leo Mei 6, 2025 jijiini Dar es Salaam, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema kampuni hizo zinapaswa kujibu hoja ndani ya siku 30 la sivyo zitafutiwa leseni zao.
Hati hizo za makosa zimetolewa rasmi kuanzia Aprili 14, 2025 na muda wake utamalizika Mei 13 mwaka huu.
“Kama wanahoja walete majibu yao, tuyahakiki tukijiridhisha na hoja zao tutawaondolea makatazo kama hawana hoja tutawafutia leseni zao kwa mujibu wa Sheria ya Madini Sura 123 ya utoaji na ufutaji wa leseni za madini na uchimbaji kifungu cha 63 na Kanuni zake, ambacho kinaeleza ukipewa leseni unapaswa uanze kazi ndani ya miezi 18,” amesema Waziri Mavunde.

Kwa mujibu wa Mavunde, Serikali imetoa leseni kwa wachimbaji wa kati na wakubwa ambazo tangu kutolewa kwake hazifanyiwa kazi.
“Zipo Kampuni tangu zimechukua leseni mwaka 2011 mpaka leo hazijaingiza hata koleo kwenye eneo miaka 14 sasa hazijaanza shughuli zozote, hatuwezi kuwa nchi ya namna hii,” amesema.
Waziri Mavunde amesema kuwa, ni leseni 7 tu kati ya 95 zikiwekwa pembeni zina mtaji wa Shilingi Trilioni 15 ambazo zimelala.
“Sisi hatuwezi kuwa nchi ambayo inatoa leseni kwa ajili ya kuchochea sekta ya madini kukua, halafu kuna watu wanachukua leseni wanakaa nazo hawafanyii kazi kwa kisingizio kuwa tupo kwenye mazungumzo na serikali na sababu mbali mbali,” ameongeza.
Sekta ya madini ni kati ya sekta zenye mchango mkubwa nchini Tanzania katika kukuza uchumi wa nchi hiyo, hasa katika kuchochea maendeleo uchumi na maendeleo ya nchi.

Comments
No comments Yet
Comment