Dollar

38,6103

0.11 %

Euro

43,8620

0.4 %

Gram Gold

4.210,4000

1.84 %

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Mahakama ya Uingereza imesema kama wakili aliyehitimu, jaji wa Mahakama Kuu ya Uganda na jaji wa Mahakama ya Uhalifu ya Umoja wa Mataifa, Lydia Mugambe alielewa sheria na akachagua kuzipuuza.

Mahakama ya UN yakataa kujihusisha na jaji wa Uganda aliyefungwa Uingereza

Mfumo wa sheria wa Umoja wa Mataifa wa Mahakama za Jinai umesema umesimamisha uhusiano na jaji wake wenye asili ya Uganda ambaye amehukumiwa Uingereza.

Lydia Mugambe, 50, amehukumiwa kifungo cha miaka sita na miezi minne katika Mahakama ya Oxford Uingereza.

Ameshtakiwa kwa kutumia wadhifa wake "vibaya" kwa kumlaghai binti mdogo kutoka Uganda kuja Uingereza mwaka 2022 na kufanya kazi za ndani bila malipo.

“Mahakama itachukua hatua zote zinazofaa za kiutawala ili kulinda zaidi uadilifu na utendakazi mzuri na utaratibu huo,” Jaji Justice Foxton wa mahakama ya Oxford Uingereza alisema.

"Hii ni kesi ya kusikitisha sana. Sasa una umri wa miaka 50 na umekuwa na tabia nzuri hapo awali. Umeshikilia wadhifa kama Jaji wa Mahakama Kuu nchini Uganda tangu 2013, na kama Jaji wa Mfumo wa sheria wa Umoja wa Mataifa wa Mahakama za Jinai tangu Mei 2023," jaji Foxton aliongezea.

Lydia Mugambe, jaji wa Mahakama Kuu ya Uganda tangu 2013, aliteuliwa mwaka 2023 kuwa jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya Umoja wa Mataifa, ambayo hufanya kazi za mahakama za awali zinazohusiana na uhalifu wa kivita uliofanywa nchini Rwanda na Yugoslavia ya zamani.

Muhula wake wa huduma ulifaa kwisha Juni 2026.

Mashtaka ya Mugambe

Mahakama inadai kuwa Mugambe alipanga kwa njia ya ulaghai viza kwa mwanamke huyo lakini iliwekwa bayana kwamba angelipwa kufanya kazi kama mtumishi binafsi katika makazi ya kidiplomasia ya John Mugerwa, naibu kamishna mkuu wa zamani wa Uganda anayeishi katika ubalozi wa nchi hiyo mjini London.

Waendesha mashtaka walisema Mugerwa alifadhili viza ya mwathiriwa akijua atafanya kazi ya utumwa kwa Mugambe.

Kwa upande wake, Mugambe angempa usaidizi kuhusiana na kesi tofauti katika mahakama ya Uganda ambayo alikuwa mshtakiwa, mahakama iliambiwa.

Mahakama ilisikiza kwamba Mugambe alilipia ndege ya mwathiriwa na kumchukua kutoka uwanja wa ndege - lakini mwanamke huyo akawa mtumwa katika nyumba ya hakimu huyo huko Kidlington, Oxfordshire.

Mahakama imempata Lydia na makosa ya kupanga njama ya uvunjaji wa sheria ya uhamiaji ya Uingereza na mtu ambaye si raia wa Uingereza, kupanga au kuwezesha safari ya mtu mwingine kwa nia ya kumnyanyasa, kuhitaji mtu kufanya kazi ya kulazimishwa au ya lazima na pia kufanya njama za kumtisha shahidi.

“Ulikutana na mwathiriwa nchini Uganda alipokuwa na umri wa miaka 19, na akipitia uzoefu ugumu mkubwa. Ulimpa mwathirika ajira na malazi kama yaya na kijakazi nchini Uganda, pamoja na kumsaidia katika masomo yake. Umeamua kumleta mwathiriwa Uingereza ili awe mlezi wa watoto na wako, ulipokuwa unamaliza masomo yako,” mashtaka dhidi ya Lydia yalisema.

Mahakama ya Uingereza imesema jaji huyo hakuwa na haki ya kisheria kama mmiliki wa viza ya mwanafunzi kumfadhili yeyote anayekuja na kumfanyia kazi Uingereza.

“Baada ya muda ulizidi kupunguza fursa za mwathirika kufanya kazi nje ya nyumba yako kwa sababu hii iliingilia kazi isiyolipwa uliyotaka akufanyie, na mwathiriwa alihisi kwamba hakuwa na njia nyingine ila kutii matakwa yako,” mahakakama imesema ikidau kuwa mwathirika ameishi kwa uwoga.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#