Dollar

42,2601

0.05 %

Euro

49,2171

0.47 %

Gram Gold

5.754,4900

1 %

Quarter Gold

9.724,2200

2.23 %

Silver

73,3300

1.33 %

Serikali ya Kenya imesema zaidi ya raia wake 200 wamejiunga na jeshi la Urusi katika vita vinayvoendelea kati ya Urusi na Ukraine, na kwamba mashirika ya ajira bado yanaendelea kutafuta Wakenya zaidi kujiunga katika mapigano.

Wakenya zaidi ya 200 wajiunga na jeshi la Urusi

Wiki iliyopita, Ukraine ilisema kuwa zaidi ya raia 1,400 kutoka nchi zipatazo thelathini za Afrika wanapigana upande wa Urusi nchini humo, baadhi yao wakiwa wameajiriwa kwa kuhadaiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andriy Sybiha, alisema Urusi inawashawishi Waafrika kusaini mikataba ambayo ni “sawa na hukumu ya kifo,” na akazitaka serikali za Afrika kuwaonya raia wao.

“Shughuli za uajiri nchini Urusi zinaripotiwa kupanuka na sasa zinawahusisha pia raia wa Kiafrika, wakiwemo Wakenya,” ilisema taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya.

Hata hivyo Ubalozi wa Urusi jijini Nairobi haukutoa ufafanuzi kuhusu hilo.

Kulingana na wizara hiyo, ubalozi wa Kenya mjini Moscow umerekodi majeraha miongoni mwa baadhi ya waajiriwa, ambao inadaiwa waliahidiwa hadi dola 18,000 ili kulipia gharama za visa, usafiri na makazi.

Msako wa usalama uliotekelezwa karibu na Nairobi mnamo Septemba uliwaokoa Wakenya 21 ambao, wizara ilisema, walikuwa wakitayarishwa kutumwa vitani. Mtu mmoja alikamatwa na anakabiliwa na mashtaka kuhusiana na tukio hilo.

Wizara hiyo ilisema kwamba waliookolewa walikuwa wamepotoshwa kuhusu aina ya kazi yao, ikiamini kuwa waliajiriwa kwa majukumu yasiyo ya vita kama vile kuunganisha ndege zisizo na rubani, na upigaji rangi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#