Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Kulingana na Rais Boko Duma wa Botswana, uamuzi huo unalenga kuhuisha idadi ya wanyamapori hao nchini India.

Duma wa Botswana aipa India zawadi ya duma 8

Rais wa Botswana, Duma Boko siku ya Jumatano, alitangaza uamuzi wa serikali yake wa kuipa India duma 8, kwa nia ya kuhuisha idadi ya wanyamapori hao ambao walipotea nchini humo miongo kadhaa iliyopita.

"Botswana itaipa India msaada wa duma 8 ili kuwasaidia kuhuisha idadi ya wanyamapori hao. Tumefanya hivyo kutokana na mafanikio yetu katika uhifadhi wa wanyamapori na mazingira," alisema Boko jijini Gaborone, baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa India, Droupadi Murmu.

Murmu yuko nchini Botswana kwa ziara ya kiserikali.

Boko alitumia fursa hiyo kumshukuru kwa Murmu kwa misaada mbalimbali ambayo India imeipa Botswana, hususani kwenye Nyanja za afya, elimu, ushirikiano wa kijeshi, biashara na uwekezaji.

"Tulikubaliana kuwa nchi hizi mbili ziendelee  kukuza ushirikiano," Boko aliongeza.

Kwa upande wake, Murmu aliishukuru Botswana kwa msaada wa wanyamapori hao, huku mataifa hayo yakiadhimisha uhusiano wa miaka 60, mwakani.

"India itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Botswana kwa lengo la kukuza ushirikiano wetu na bara la Afrika," alisema Murmu.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#