Sport
Dollar
42,2398
0.03 %Euro
48,9861
0.07 %Gram Gold
5.716,7800
1.97 %Quarter Gold
9.512,1700
-0.01 %Silver
72,8700
4.75 %Serikali ya DRC ilitoa hati yake ya kukamatwa kwake mwaka 2011 baada ya kuhusishwa na kukiunga mkono kikundi cha waasi cha M23, na kulazimika kukimbilia nchini Ufaransa.
Shauri linalomkabili kiongozi wa zamani wa waasi nchini DRC Roger Lumbala, limeanza kusikilizwa jijini Paris.
Lumbala anashitakiwa kwa kushiriki uhalifu dhidi ya binadamu, wakati wa mgogoro wa kisiasa kati yam waka 1998 na 2008, nchini DRC.
Kiongozi huyo wa waasi anakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani, hukumu ambayo inatarajiwa kutolewa Disemba 19.
Lumbala, mwenye umri wa miaka 67, aliongoza kikundi cha waasi kiitwacho Congolese Rally for National Democracy, kilichokuwa kikiungwa mkono na Uganda, kikituhumiwa kwa kutesa raia, hususani wale kutoka jamii za Nande na Mambuti.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, kikundi hicho kilitesa watu pamoja na kufanya vitendo vya ubakaji.
Baada ya vita hivyo, Lumbala alihudumu kama Waziri wa Biashara ya Nje, katika serikali ya mpito ya DRC, kati ya mwaka 2003 na 2005 kabla hajateuliwa kuwa mbunge.
Serikali ya DRC ilitoa hati yake ya kukamatwa kwake mwaka 2011 baada ya kuhusishwa na kukiunga mkono kikundi cha waasi cha M23, na kulazimika kukimbilia nchini Ufaransa.
Comments
No comments Yet
Comment