Dollar

42,2473

0.06 %

Euro

48,9455

-0.01 %

Gram Gold

5.610,6400

0.08 %

Quarter Gold

9.515,6500

0.02 %

Silver

70,2900

1.03 %

Libya imetakiwa na Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne kufunga vituo vya kuwazuiliia wahamiaji ambapo mashirika ya haki za binadamu yanasema wahamiaji na wakimbizi wamekuwa wakiteswa, kunyanyaswa na wakati mwingine kuuawa.

Libya yatakiwa kufunga vituo vya kuwazuilia wahamiaji katika mkutano wa Umoja wa Mataifa

Mataifa mengi yakiwemo Uingereza, Hispania, Norway na Sierra Leone yameonyesha wasiwasi wao katika mkutano wa Geneva kuhusu masaibu ya wahamiaji nchini Libya, ambayo ni njia kuu ya kupita kwa Waafrika wanaokimbia migogoro na umaskini kuelekea Ulaya.

Baadhi yao wamezuiliwa kwenye maghala na wanaosafirisha watu kinyume na sheria ambapo wamekuwa wakikabiliwa na ghasia na dhulma, kulingana na kesi ya mahakama ya Uholanzi.

Balozi wa Norway Tormod Endresen alitoa wito wa ulinzi wa wahamiaji walio katika mazingira magumu na kukomeshwa kwa kuwekwa kizuizini kiholela.

Balozi wa haki za Uingereza Eleanor Sanders aliunga mkono hilo na pia akatoa wito wa ufikiaji usiozuiliwa kwa Umoja wa Mataifa na makundi mengine kwenye makaburi ya halaiki.

Baadhi ya miili ya wahamiaji iliyopatikana kwenye makaburi ya halaiki mapema mwaka huu ilikuwa na majeraha ya risasi, shirika la Umoja wa Mataifa lilisema.

Katika barua ya wazi kwa mamlaka ya Libya iliyochapishwa sanjari na tathmini ya Umoja wa Mataifa, mashirika ya haki za binadamu yalitaka marekebisho, yakisema kwamba makundi yenye silaha yanafanya kazi bila kuadhibiwa, kuzuia mahakama na kufanya ukiukwaji mkubwa.

Libya imekuwa na changamoto ya amani tangu uasi wa mwaka 2011 dhidi ya kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi.

Eltaher Salem M. Elbaour wa Libya, Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Serikali ya Magharibi inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa yenye makao yake makuu katika mji mkuu Tripoli, alisema wahamiaji waliweka mzigo mkubwa kwa taifa hilo lililogawanyika.

"Siko hapa kutoa taswira kamili ya hali ya haki za binadamu katika nchi yangu," alisema. "Kinyume chake kabisa - nimekuja hapa kusisitiza juhudi kubwa tulizofanya ili kuhakikisha haki hizi zinaheshimiwa licha ya changamoto ambazo zinajulikana kwa wote katika kipindi hiki cha mpito."

Alitoa mfano wa nchi yake kukubali mamlaka ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu nchini Libya na kuundwa kwa kamati mpya ya pamoja ya kushughulikia vituo vya wafungwa.

Tathmini ya Libya ni sehemu ya mchakato ambao serikali na makundi ya haki za binadamu huchunguza rekodi zote 193 za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kila baada ya miaka michache na kupendekeza uboreshaji.

Marekani ilipuuza tathmini yake wiki iliyopita katika hatua isiyo ya kawaida.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#