Kulingana na Mudavadi, Wakenya 34 wanatibiwa mahospitalini, hyku 62 wakirudishwa nyumbani, na watano wakiwa ni wafungwa wa kivita.
Waziri wa Mambo ya Nje ya Kenya, Musalia Mudavadi, amesema kuwa, jumla ya raia 84 wa nchi hiyo, wanaripotiwa kuuawa katika vita kati Urusi na Ukraine.
Akizungumza mbele ya kamati ya Seneti inayoshughulikia ajira na ulinzi, Mudavadi alisema kuwa, Wakenya wapatao 354, wamehusika na mgogoro kati ya nchi hizo mbili.
“Wizara yetu ina rekodi ya Wakenya 354 ambao wamehusishw ana mgogoro kati ya Urusi na Ukraine,” aliwaambia maseneta wa nchi hiyo.
“Kwenye mstari wa mbele, tuna taarifa za Wakenya 77, huku wengine 38 wakiwa kambini. 52 hawajulikani walipo wakati 84, wanahofiwa kupoteza maisha.”
Kulingana na Mudavadi, Wakenya 34 wanatibiwa mahospitalini, hyku 62 wakirudishwa nyumbani, na watano wakiwa ni wafungwa wa kivita.
Aliongeza kuwa, baadhi ya familia zimewasiliana na serikali ya nchi hiyo, baada ya kupoteza mawasiliano na ndugu zao walioko Urusi.
“Nitoe raia kwa wanafamilia kuendelea kushirikiana na wizara yetu mapema iwezekanavyo,” alisema.
