Sudan Kusini iko katika maandalizi ya kufanya Uchaguzi Mkuu wa kwanza tangu nchi hiyo kupata uhuru 2011.
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amejiandikisha katika daftari la mpiga kura katika Kituo cha Kujiandikisha cha Hai Gonya, Jimbo nambari 1, mjini Juba.
Baada ya kukabidhiwa kadi yake ya kupiga kura, aliwataka raia wa nchi hiyo wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi, kujisajili na kuchukua kadi zao.
Sudan Kusini iko katika maandalizi ya kufanya Uchaguzi Mkuu wa kwanza tangu nchi hiyo kupata uhuru 2011.
Tarehe ya awali iliyopangwa ilikuwa ni Disemba, 2026, hata hivyo, tarehe hiyo imesogezwa mbele hadi mwezi Februari 2027.
Kwa upande wake, Rais mstaafu wa Tanzania ambae pia ni Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Afrika (AU) katika Pembe ya Afrika na Bahari ya Sham, Jakaya Kikwete, ameutaka Umoja wa Mataifa na Jumuia ya Kimataifa kuisadia Sudan Kusini kifedha na kiusalama ili taifa hilo changa liweze kufanya Uchaguzi Mkuu kwa amani.
Kikwete alitoa wito huo Novemba, 2026 alipokuwa akizungumza kwa njia ya video na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
TRT Afrika — TRT Afrika
Afrika
