Dollar

42,9259

0.13 %

Euro

50,6303

-0.18 %

Gram Gold

6.252,4200

1.32 %

Quarter Gold

10.319,2000

1 %

Silver

108,1200

9.12 %

Hatua ya Israel ni kile ambacho Uturuki inaona kuwa sehemu ya sera zake za kukalia maeneo na kuzuia juhudi za kutambuliwa kimataifa kwa Taifa la Palestina, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki Oncu Keceli amesema.

Uturuki yashtumu Israel kutambua Somaliland kama kinyume cha sheria, kuzua taharuki

Uturuki imeshtumu hatua ya Israel ya kutambua jimbo la Somalia lililojitenga la Somaliland kama taifa huru, kuiita kuwa ni kinyume cha sheria ambayo itatatiza usalama wa eneo hilo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Oncu Keceli alisema siku ya Ijumaa kuwa uamuzi wa Israel ni “mfano mwingine wa vitendo vya kinyume cha sheria vya serikali ya Netanyahu vinavyolenga kusababisha ukosefu wa usalama katika ngazi ya kanda na duniani,” akiongeza kuwa huu ni “uingiliaji wa wazi wa masuala ya ndani ya Somalia”.

Alisema hatua ya Israel ilikuwa sehemu ya kile Uturuki inaona sera za kukalia maeneo na juhudi za kuzuia kutambuliwa kimataifa kwa Taifa la Palestina.

Keceli alisisitiza kuwa maamuzi kuhusu mustakbali wa Jamhuri ya Somalia na eneo la Somaliland lazima yachukuliwe kwa njia ambayo inazingatia “utashi wa Wasomali wote”.

Shutuma hizi zinakuja wakati Israel siku ya Ijumaa ilipotangaza kuwa inatambua rasmi Somaliland kama taifa huru.

Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu anasema hatua hii imefanyika kwa mujibu wa “makubaliano ya Abraham,” katika makubaliano yaliyotiwa saini 2020 kuimarisha uhusiano kati ya Israel na UAE, Bahrain, Sudan na Morocco.

Netanyahu pia alimualika rais wa Somaliland kufanya ziara rasmi nchini Israel.

Akisisitiza kuunga mkono kwa Uturuki juu ya uhuru wa mipaka ya Somalia, Keceli alisema Uturuki, ambayo inalipa umuhimu mkubwa suala la amani na usalama katika Pembe ya Afrika, itaendelea kusimama na watu wa Somalia.

Kwingineko, Misri pia ilisema siku ya Ijumaa kuwa mawaziri wa mambo ya nje wa Somalia, Misri, Uturuki na Djibouti wameshtumu uamuzi huo.

"Mawaziri wamesisitiza kukataa kwao kikamilifu na kushtumu hatua ya Israel kutambuwa eneo la Somaliland, wakisisitiza kuunga mkono kikamilifu umoja, uhuru na uhuru wa mipaka ya Somalia," Wizara ya mambo ya nje ya Misri ilisema katika taarifa kufuatia mazungumzo kwa njia ya simu kati ya waziri wa mambo ya nje wa Misri na wenzake wa Somalia, Uturuki na Djibouti.

Somaliland ilijitangazia uhuru kutoka kwa Somalia 1991 lakini haijapata kutambuliwa kimataifa.

Licha ya kuwa na utawala wao wenyewe, Somalia inatizama eneo hilo kama sehemu muhimu ya taifa lake na kuona ushirikiano wowote wa moja kwa moja na Somaliland kama ukiukwaji wa uhuru na umoja wao.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#