Dollar

42,8673

0.03 %

Euro

51,0115

0.17 %

Gram Gold

6.226,5100

0.9 %

Quarter Gold

10.216,8600

0 %

Silver

102,2800

3.23 %

Tume ya Kupambana na Rushwa ya Zambia (ACC) imempongeza polisi wa kike aliyekataa rushwa ya dola $50,000 kutoka kwa mshukiwa wa utakatishaji fedha katika uwanja wa ndege mji mkuu wa Lusaka.

Polisi akataa rushwa ya dola $50,000 katika uwanja wa ndege nchini Zambia

Tume ya Kupambana na Rushwa nchini Zambia (ACC) imempongeza polisi wa kike aliyekataa rushwa ya dola $50,000 kutoka kwa mshukiwa wa utakatishaji fedha katika uwanja wa ndege wa mji mkuu, Lusaka.

Sajini Ruth Nyambe, ambaye yuko kwenye Kitengo cha Viwanja vya Ndege, alikataa pesa hizo kutoka kwa mshukiwa, wakati wa taratibu za kiusalama, na inadaiwa mshukiwa huyo alipatikana akiwa na dola milioni $2.3 taslimu na vipande vinavyoaminika kuwa vya dhahabu visaba katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda.

Polisi nchini Zambia wanasema tukio hilo lilifanyika Februari 5, 2025.

ACC ilisema kuwa mshukiwa huyo ambaye jina lake halikutajwa alitaka kumhonga Nyambe dola $5,000 kwanza, lakini alipokataa, mshukiwa huyo akapandisha dau hadi dola $50,000 ili aruhusiwe aendelee na safari yake na fedha hizo.

'Uadilifu wa hali ya juu'

Kwa mara nyingine tena, Nyambe akakataa, na badala yake kuwafahamisha maafisa wa Tume ya Kupambana na Dawa za Kulevya ya Zambia (DEC), na mshukiwa akakamatwa.

Mshukiwa huyo alikuwa anasafiri kutoka Lusaka hadi sehemu ambayo haikufahamika, kulingana na Lusaka Times.

ACC ilimpongeza Nyambe na kusema kuwa ni polisi "mwenye weledi wa juu" katika majukumu yake.

Work promotion

Mkurugenzi Mkuu wa ACC Daphne Chabu alimtunukia Nyambe na tuzo ya Uadilifu. Haikufahamika kama pia kulikuwa na zawadi ya fedha.

Siku ya Jumatano, Inspekta Jenerali wa Polisi wa Zambia Graphel Musamba alimpandisha cheo Nyambe hadi Mkaguzi wa Polisi, kutoka kuwa Sajini.

Polisi inasema kupandishwa cheo kwa Nyambe kunaendana na "kutambua uadilifu wake, utendaji kazi, na kukataa kupokea rushwa."

Kwingineko, Inspekta Jenerali Musamba alimpandisha cheo Sajini Samuel Mbewe hadi kuwa Mkaguzi wa Polisi baada ya kukataa rushwa ya Kwacha za Zambia 20,000 ( dola $890) kutoka kwa raia wa kigeni.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#