Sport
Dollar
42,8515
0.01 %Euro
50,9195
0.01 %Gram Gold
6.170,8800
0 %Quarter Gold
10.216,8600
-0.28 %Silver
99,0800
0.11 %Uturuki pia itaangazia hali ya rubani, ubora wa kiufundi, rekodi za ndege, ikiwemo vipuri.
Uchunguzi kuhusu ajali ya ndege iliyomuua mkuu wa majeshi wa Libya na watu wengine saba siku ya Jumanne umeanzishwa na ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Ankara, vyanzo na maaafisa wamewaambia Anadolu.
Uchunguzi unafanywa kwa usimamizi wa naibu mwendesha mashtaka mkuu na waendesha mashtaka wengine wanne.
Ndege hiyo ya kibiashara aina ya Falcon 50 ilianguka baada ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Esenboga jijini Ankara kuelekea mji mkuu wa Libya, Tripoli.
Ndege hiyo ilipatikana karibu kilomita 2 kusini mwa kijiji cha Kesikkavak katika wilaya ya Haymana ya mkoa wa Ankara.
Upasuaji wa maiti, utaratibu wa kulala, matengenezo — kila kitu kitachunguzwa
Kama sehemu ya uchunguzi, vyanzo hivyo vimesema, eneo ambalo ndege hiyo ilianguka limezungushiwa ua wa ulinzi na linalindwa muda wote.
Mabaki yote ya ndege, hasa kisanduku cha mawasiliano, kinachoaminika kuwa muhimu zaidi kwenye ajali hiyo, yamehifadhiwa sehemu salama.
Wakati huohuo, vipimo vya upasuaji wa maiti vinafanywa kubaini chanzo mahsusi cha vifo vya wale waliokuwa kwenye ndege.
Shughuli za kuandaa miili zinaendelea katika Kurugenzi ya Taasisi ya Tiba ya Ankara.
Wachunguzi wanafuatilia kwa karibu hali ya marubani kabla ya ajali hiyo.
Anadolu imebaini kuwa kila kitu kinachohusiana na ajali hiyo kinafanyiwa tathmini, ikiwemo utaratibu wa kulala wa wahudumu wa ndege, vyakula, uwezekano wa kunywa pombe au kutumia dawa, na hali yao ya kisaikolojia kwa ujumla.
Uchunguzi unaweza kuwa zaidi
Ofisi ya mwendesha mashtaka pia imeomba ripoti ya wataalamu ya kiufundi kubaini kama ndege ilikuwa iko sawa kufanya kazi.
Jukumu na matatizo yoyote ya kiufundi ya waliohusika kuifanyia matengenezo ndege hiyo siku za hivi karibuni litatathminiwa kwa makini.
Katika kufanya uchunguzi, kamera za uwanja wa ndege zimechukuliwa kuangaliwa kwa makini, na mawasiliano yote kwa njia ya redio kati ya kituo cha kuongoza ndege na ndege yameongezwa kwenye uchunguzi huo.
Imefahamika kuwa tathmini ya kiufundi itaongezwa kwenye uchunguzi huo kubaini kama vipuri vilivyotumika wakati wa matengenezo vinaendana na viwango vinavyotakiwa.
Wakati huohuo, sampuli zimechukuliwa kutoka kwa tenki la mafuta na mabaki ya ndege kuondoa hofu ya mafuta kuchakachuliwa au matumizi ya mafuta yasiyo sahihi.
Taarifa za hali ya hewa wakati ndege ilipoanguka katika eneo hilo zimeombwa.
Mamlaka zinapendekeza kuwa kama uchunguzi utabaini kuwa ajali ilisababishwa na makosa ya utengenezaji, jukumu la msururu wa watakaowajibishwa litakuwa pana zaidi.
Comments
No comments Yet
Comment