Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Baadhi ya raia wa Kenya walilalamika siku ya Jumatano baada ya tembo waliokuwa wakiranda randa kuwaua watu wanne katika kipindi cha wiki moja kwa kile wataalamu wanaeleza mzozo kati ya binadamu na wanyamapori unaosababishwa na uhaba wa malisho.
Baadhi ya raia wa Kenya walilalamika siku ya Jumatano baada ya tembo waliokuwa wakiranda randa kuwaua watu wanne katika kipindi cha wiki moja kwa kile wataalamu wanaeleza mzozo kati ya binadamu na wanyamapori unaosababishwa na uhaba wa maeneo ya malisho.
Tembo au ndovu mmoja anayeaminika kuwaua watu wawili alipigwa risasi katika Kaunti ya Kajiado. Shirika la Wanyamapori la Kenya limetoa wito wa kuwepo kwa utulivu.
“Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa ndovu waliofanya hivyo wana majeraha yanayotokana na kuchomwa mishale na mikuki, kuashiria kulikuwa na makabiliano,” shirika hilo lilisema kwenye taarifa.
Wakazi wameripoti kuongezeka kwa idadi ya tembo wanaoranda randa eneo la Ole Tepesi katika Kaunti ya Kajiado, kwa kile wataalamu wanachosema ni kugombania raslimali. Kenya imepata mvua kidogo katika msimu wa mvua za vuli.
Shirika la Wanyamapori laahidi kuchukuwa hatua zaidi
Mamlaka za eneo hilo zimesema kuwa waliouawa hivi karibuni ni mwanamume mmoja aliyekuwa akichunga mbuzi siku ya Jumanne.
Shirika la Wanyamapori la Kenya (KWS) limeahidi “kuimarisha mikakati zaidi, ili kukabiliana na hali hiyo mapema na kupunguza hatari za matukio hayo katika siku zijazo.”
Serikali ya Kenya ina mpango wa kulipa fidia ambapo maelfu ya watu waliojeruhiwa au kuuawa na wanyamapori wamelipwa mamilioni ya shilingi za Kenya katika kipindi cha miaka michache iliopita.
Comments
No comments Yet
Comment