Sport
Dollar
42,8445
0.05 %Euro
50,6848
-0.09 %Gram Gold
6.170,4000
-0.36 %Quarter Gold
10.245,1600
0.39 %Silver
98,9700
0.47 %Recep Tayyip Erdogan ametoa salamu zake za rambirambi kwa Abdul Hamid Dbeibah katika mazungumzo kwa njia ya simu baada ya ajali ya ndege jijini Ankara iliyosababisha kifo cha mkuu wa majeshi ya Libya, mkurugenzi wa mawasiliano wa Uturuki amesema.
Rais wa Uturuki amezungumza kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Libya, akitoa salamu zake za rambirambi kutokana na ajali iliyosababisha kifo cha mkuu wa majeshi ya Libya nchini Uturuki, kulingana na mkurugenzi wa mawasiliano wa Uturuki Burhanettin Duran.
Wakati wa mazungumzo hayo na Abdul Hamid Dbeibah siku ya Jumatano, Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki “alieleza huzuni wake na majonzi kuhusu kupotea kwa maisha katika ndege iliyokuwa imembeba mkuu wa majeshi ya Libya, Jenerali Mohammed Ali Al-Haddad, na wale waliokuwa wameongozana naye,” alisema Duran.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya awali alisema mabaki ya ndege hiyo aina ya Falcon 50 ya kibiashara, ambayo iliondoka kutoka Uwanja wa Ndege wa Esenboga jijini Ankara kuelekea Tripoli Jumanne, yalipatikana na maafisa wa usalama karibu kilomita 2 kusini mwa Kesikkavak katika wilaya ya Haymana ya Ankara.
Kisanduku cha ndege hiyo na kifaa cha kurekodi sauti vilipatikana siku ya Jumatano, Yerlikaya alisema.
Shughuli ya kutathmini vifaa hivyo kubaini chanzo cha ajali hiyo imeanza, aliongeza.
Kufuatia vifo hivyo, Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.
Comments
No comments Yet
Comment