Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Yasar Guler, Mkuu wa Majeshi Bayraktaroglu walitoa salamu zao za rambirambi kwa maafisa wa Libya na familia zao baada ya ajali ya ndege
Wzziri wa Ulinzi wa Uturuki Yasar Guler amewatembelea kuwafariji maafisa waliowasili jijini Ankara kupokea miili ya ujumbe wa jeshi la Libya ambao ulikuwa kwenye ndege iliopta ajali siku ya Jumanne.
Katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Uturuki NSosyal, wizara hiyo imesema kuwa maafisa wa kijeshi wa Libya na familia za wale waliopoteza maisha wamefika Uturuki kuchukuwa miili yao.
Taarifa hiyo imesema kuwa Mkuu wa Majeshi wa Uturuki Jenerali Selcuk Bayraktaroglu pia aliwatembelea kuwafariji maafisa wa Libya na familia. Wote Guler na Bayraktaroglu walieleza huzuni yao kuhusu ajali hiyo na kutoa salamu za rambirambi kwa familia pamoja na watu wa Libya.
Siku ya Jumanne, ndege aina ya Falcon 50-ya kibiashara ilianguka baada ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Esenboga jijini Ankara kuelekea mji mkuu wa Libya, Tripoli.
Ndege hiyo ilipatikana karibu kilomita 2 (maili 1.24) kusini mwa Kesikkavak katika wilaya ya Haymana ya mji mkuu wa Uturuki, Ankara.
Shughuli za kutafuta ziliendelea usiku kucha licha ya mvua kubwa na ukungu, na maafisa wanafuatilia juhudi hizo kupitia kituo cha kuratibu kilichowekwa na shirika la kukabiliana na majanga la Uturuki AFAD.
Comments
No comments Yet
Comment