Dollar

42,8833

-0.05 %

Euro

50,9195

0.01 %

Gram Gold

6.169,7300

-0.01 %

Quarter Gold

10.245,1600

0 %

Silver

99,0700

0.09 %

Wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) wanadai kuchukuwa udhibiti wa maeneo mawili katika jimbo la magharibi mwa Sudan la Darfur Kaskazini.

RSF yadai kuchukuwa udhibiti wa maeneo mawili katika eneo la Sudan la Kaskazini mwa Darfur

Wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) wanadai kuchukuwa udhibiti wa maeneo mawili katika jimbo la magharibi mwa Sudan la Darfur Kaskazini.

Vikosi vya RSF, vikiwa na magari ya kadhaa ya kivita, vilishambulia Abu Qamra, ulioko karibu kilomita 200 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa mkoa wa Al Fasher, vyanzo vya eneo hilo viliiambia Anadolu.

Eneo hilo limekuwa chini ya udhibiti wa jeshi la Sudan na vikosi washirika.

Kulingana na vyanzo hivyo, vikosi vya RSF pia vilishambulia mji wa Ambro, karibu kilomita 300 kaskazini magharibi mwa Al Fasher.

Video

Kundi hilo la wapiganaji limesema katika taarifa kuwa wapiganaji wake ‘‘wamedhibiti vizuri” maeneo yote mawili.

Wapiganaji wa RSF waliweka video kwenye mtandao wa kijamii ambazo zinaonesha wao kuwepo kwenye maeneo hayo.

Hakukuwa na taarifa yoyote kutoka kwa jeshi la Sudan kuhusu madai hayo.

Kati ya majimbo 18 ya Sudan, RSF inadhibiti majimbo matano ya eneo la Darfur magharibi mwa nchi, isipokuwa maeneo fulani ya Darfur Kaskazini ambayo bado yanadhibitiwa na jeshi.

Vita vimewaua maelfu ya watu

Jeshi, linadhibiti maeneo mengine ya majimbo 13 kusini, kaskazini, mashariki, na kati, ikiwemo mji mkuu wa Khartoum.

Mapigano hayo kati ya jeshi la Sudan na RSF, yaliyoanza Aprili 2023, yameua maelfu ya watu tangu wakati huo na kusababisha mamilioni wengi kukimbia makazi yao.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#