Sport
Dollar
42,9314
0.18 %Euro
50,6706
0.02 %Gram Gold
6.226,7800
0.91 %Quarter Gold
10.283,8000
0.66 %Silver
102,8400
3.79 %Rais wa Marekani amesema nchi yake ilifanya mashambulizi mengi yaliyolenga shabaha dhidi ya Daesh nchini Nigeria.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria ilithibitisha siku ya Ijumaa kuwa mashambulizi ya angani yaliyofanya na Marekani dhidi ya magaidi yalilenga shabaha katika eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, na ikaongeza kuwa bado inaendelea kushirikiana katika masuala ya kiusalama na Marekani.
Usiku wa kuamkia Ijumaa Rais wa Marekani amesema nchi yake ilifanya mashambulizi mengi yaliyolenga shabaha dhidi ya Daesh kaskazini-magharibi mwa Nigeria, akidai kuwa kundi hilo limekuwa likiwalenga Wakristo.
“Usiku wa leo, kwa maelekezo yangu kama Amiri Jeshi Mkuu, Marekani ilianzisha shambulizi kali dhidi ya magaidi wa ISIS (Daesh) kaskazini-magharibi mwa Nigeria, ambao wamekuwa wakilwalenga na kuwaua kikatili, hasa Wakristo wasio na hatia,” Trump alisema kupitia mtandao wa kijamii wa Truth Social siku ya Alhamisi.
“Nilikuwa nimewaonya magaidi hawa hapo awali kwamba kama hawataacha mauaji ya Wakristo, kutakuwa na adhabu kali, na usiku wa leo, adhabu hiyo imetolewa.”
Aliongeza kuwa “hilo ni jambo ambalo ni Marekani pekee inayoweza kulifanya.”
Hata hivyo mamlaka za Nigeria na watafiti wamekuwa wakipinga mara kwa mara madai ya Trump kwamba magaidi wanawalenga Wakristo hasa nchini Nigeria, wakisema kuwa makundi ya kigaidi hufanya mashambulizi bila kubagua raia, bila kujali dini zao.
Kuonyesha ubabe wa Marekani
Kamandi ya Marekani barani Afrika (AFRICOM) ilisema kupitia mtandao wa kijamii wa X kwamba shambulizi hilo lilifanywa kufuatia ombi la mamlaka za Nigeria.
“AFRICOM ilifanya shambulizi kufuatia ombi la mamlaka za Nigeria katika Jimbo la Sokoto, na kuwaua magaidi kadhaa wa ISIS (Daesh),” AFRICOM ilisema, ikiashiria Jimbo la Sokoto lililoko kaskazini-magharibi mwa Nigeria.
“Mashambulizi haya makali dhidi ya ISIS yanaonyesha nguvu ya jeshi letu na dhamira yetu ya kuondoa vitisho vya kigaidi dhidi ya Wamarekani ndani na nje ya nchi.”
Serikali ya Nigeria hapo awali ilisema kuwa makundi yenye silaha huwalenga Waislamu na Wakristo kwa pamoja. Hata hivyo, Trump alidai mwezi Oktoba kwamba Wakristo wanakabiliwa na “tishio la kuwepo” nchini humo.
Mapema wiki hii, shirika la habari la Reuters liliripoti kuwa Marekani imekuwa ikikusanya taarifa za kijasusi juu ya maeneo ya Nigeria tangu mwishoni mwa Novemba.
Comments
No comments Yet
Comment