Dollar

42,9307

0.18 %

Euro

50,6328

-0.09 %

Gram Gold

6.245,4700

1.21 %

Quarter Gold

10.319,2000

1 %

Silver

107,6600

8.66 %

Vikosi hivyo vinashtumu kundi hilo la wapiganaji wa RSF kwa kuchoma moto vijiji, kupora mali

Vikosi washirika vya jeshi la Sudan vinasema vimetibuwa mashambulizi ya RSF Darfur Kaskazini

Kundi lenye silaha ambalo ni washirika wa jeshi la Sudan siku ya Alhamisi lilisema kuwa limefanikiwa kutibuwa shambulizi la wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF) katika maeneo kadhaa jimbo la Darfur Kaskazini magharibi mwa Sudan.

Vikosi hivyo vinavyoshirikiana Darfur vilisema katika taarifa kuwa vimekabiliana na mashambulizi ya RSF katika baaadhi ya maeneo ya Darfur Kaskazini, hasa karibu na Abu Qumra, vikishtumu wapiganaji wa RSF kwa kuendeleza mashambulizi dhidi ya raia wasio na silaha.

Vikosi hivyo vinasema kuwa RSF inataka kudhibiti eneo hilo “kwa lazima kupitia mauaji, kuondoa watu katika makazi yao na kutesa raia pamoja na watu walioondoka katika makazi yao wakikimbia mapigano katika mji wa El-Fasher,” makao makuu ya jimbo, taarifa hiyo iliongeza.

Vyanzo vya eneo hilo vinasema RSF ilishambulia maeneo ya Abu Qamra na Ambro siku ya Jumatano.

Vikosi washirika vya jeshi vinasema tangu mashambulizi hato kuanza, RSF imechoma vijiji vyote, kuiba mifugo na mali za watu, na kukiuka haki dhidi ya wakazi.

RSF ilianza mashambulizi yake mapema siku ya Alhamisi katika eneo hilo, lakini vikosi vilivyokuwa vinalinda vilifanikiwa kutibuwa mashambulizi hayo tena, na kuwakabili vikali wapiganaji hao, magari yao na vifaa kuwalazimisha kurudi nyuma, vikosi hivyo washirika vilisema.

Mashambulizi hayo yanakuja huku RSF ikitaka kuchukuwa udhibiti kamili wa Darfur Kaskazini. Jeshi la Sudan na vikosi washirika linadhibiti maeneo matatu kwenye jimbo hilo — Ambro, Karnoi na Tina — huku Sudan Liberation Movement inayoongozwa na Abdel Wahid al-Nur likidhibiti eneo la Tawila.

Mapigano yalitokana na RSF kuchukuwa udhibiti wa El-Fasher Oktoba 26, ambapo mashirika ya maeneo hayo na kimataifa yameripoti mauaji ya kikatili kwa raia, kusababisha onyo kutolewa kuhusu hatari ya mgawanyiko zaidi nchini Sudan.

Majimbo matatu ya Kordofan—Kaskazini, Magharibi, na Kusini —yamepitia wiki kadhaa za mapigano makali kati ya jeshi na RSF, kulazimisha maelfu ya watu kukimbia maeneo hayo.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na RSF, ambayo yalianza Aprili 2023, yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na mamilioni wengine kuondoka katika makazi yao.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#