Dollar

42,9259

0.13 %

Euro

50,6303

-0.18 %

Gram Gold

6.252,4200

1.32 %

Quarter Gold

10.319,2000

1 %

Silver

108,1200

9.12 %

Balozi Fathudin Ali Ospite anasema msaada wa Uturuki ulichangia “pakubwa” kuhakikisha mji mkuu Mogadishu uko salama, na kufanikisha upigaji kura.

Balozi wa Somalia nchini Uturuki apongeza mchango wa  Uturuki kwa usalama uchaguzi wa kihistoria

Balozi wa Somalia nchini Uturuki amepongeza ushirikiano wao na Uturuki kwa kusaidia kupata mafanikio katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika siku ya Alhamisi katika jimbo la Somalia la Banadir, ambalo linajumuisha mji mkuu, Mogadishu.

Balozi Fathudin Ali Ospite anasema msaada wa Uturuki ulichangia “pakubwa” kuhakikisha kuna hali ya usalama katika mji mkuu na kufanikisha uchaguzi wa kwanza ambapo raia walishiriki kuwahi kufanyika katika mji huo ndani ya kipindi cha zaidi ya miongo mitano.

Aliuelezea uchaguzi huo kama “hatua muhimu” katika mchakato wa kurudisha mfumo wa demokrasia.

“Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Jamhuri ya Uturuki, taifa la kuaminika na lenye undugu, ambalo limeendelea kutuunga mkono, haswa kuhakikisha usalama katika mji wetu mkuu kwenye miaka ya hivi karibuni, limekuwa na jukumu muhimu kuwezesha mchakato wa kidemokrasia,” balozi huyo aliiambia TRT Afrika.

“Umoja wao na Somalia umeimarisha imani kwa umma na kuhakikisha hatua hii muhimu inafanikiwa.”

Uchaguzi wa Alhamisi ni wa kwanza tangu wakazi wa Mogadishu kupiga kura kuchagua viongozi wao 1969, kuondokana na mfumo wa ukoo kuteua watu katika miongo ya hivi karibuni.

Maelfu ya waliojisajili kupiga kura walipiga foleni katika vituo mbalimbali kuchagua viongozi wao.

Wengi ya wapiga kura hao walikuwa vijana ambao walizaliwa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya nchi hiyo na walikuwa wanapiga kura kwa mara ya kwanza, kulingana na Balozi Ospite. Alisema mazingira kote katika mji mkuu siku ya uchaguzi yalikuwa ya umoja na uthubutu.

“Kwa miongo kadhaa, watu wetu wametaka haki ya kuchagua viongozi wao kwa uhuru wala siyo kugawanywa, tofauti na mfumo ambao wamepandikiziwa na kutokuwa na hofu ,” balozi alisema. “Kuwa sasa hofu haipo tena.”

Balozi huyo alielezea uchaguzi huo kama msingi wa kuelekea kupata utulivu wa taifa.

“Kupitia amani, haki za kidemokrasia na uhuru wa kuchagua viongozi, Somalia inaweka msingi wa maendeleo ya muda mrefu — kukuwa kwa uchumi, ustawi wa jamii, na mafanikio kwa taifa,” alisema.

Hongera kwa hatua muhimu

Mabalozi wa Somalia kote duniani wamempongeza Rais Hassan Sheikh Mohamud, serikali na raia kwa hatua hiyo muhimu.

Ubalozi wa Somalia nchini Uturuki umesisitiza kuwa mafanikio ya usalama kwa siku hiyo yamedhihirisha dhamira ya mataifa yote mawili na ushirikiano wa kimataifa.

“Kama taifa mabalo wakati mmoja lilitambulika kwa makabidhiano ya amani ya madaraka, tumechukuwa hatua muhimu kurudisha urithi huo,” balozi huyo alisema.

Ubalozi wa Somalia nchini Tanzania pia ulituma pongezi zake kwa uchaguzi wa amani katika mji mkuu wa nchi.

Katika taarifa, iliitaja siku hiyo kama siku ya ushindi kwa utashi wa taifa. Ubalozi huo pia unawakilisha Somalia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na pia unahudumia mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Malawi, Rwanda,Visiwa vya Comoro, na Mauritius.

“Hii ni siku ya kihistoria kwa Somalia, kwa kuwa taifa letu linafanya uchaguzi wake kwa njia ya amani huku raia wakihusika moja kwa moja katika kipindi cha zaidi ya miaka 57,” taarifa hiyo ilisema.

Ubalozi huo ulielezea mafanikio ya uchaguzi huo kutokana na “uthubutu wa watu wa Somalia” na “uongozi imara” wa Rais Mohamud.

“Mafanikio haya yanaonesha hatua ya dhati ya kurudi kwenye demokrasia, uthabiti na maendeleo kwa taifa letu tunalolipenda,” ubalozi ulieleza.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#