Mkataba huo, utaupa Misri utawala mkubwa katika sekta ya bahari, ukilinganisha na ule ambao unapanga kusaini na Ugiriki.
Wizara ya Ulinzi ya Uturuki imesema kuwa ipo tayari kuingia mkataba wa bahari na Misri.
"Kwa mara nyingine tena, tunasisitiza kuwa tupo tayari kusaini mkataba huo na Misri, kwa maslahi ya pande mbili,” ilisema wizara hiyo kupitia taarifa yake.
Mkataba huo, utaupa Misri utawala mkubwa kwenye sekta ya majini, ukilinganisha na ule ambao unapanga kusaini na Ugiriki.
"Baada ya tathimini, tumegundua kuwa Misri itavuna zaidi ya kilomita za mraba 15,000 ya utawala katika eneo la bahari."
Kulingana na wizara hiyo, Uturuki itaendelea kulinda maslahi yake katika eneo la Mashariki ya Mediterenia.
Kwa upande mwingine, wizara hiyo imeipongeza Libya kwa kuidhinisha makubaliano ya maelewano na Uturuki.
Yapongeza jitihada za kuimarisha usalama katika eneo la Sinjar
Msemaji wa wizara hiyo, Zeki Akturk alipongeza jitihada za serikali ya Iraq za kuimarisha utawala wake na kurejesha hali ya kawaida katika eneo la Sinjar.
"Ni hatua nzuri kumaliza uwepo wa magaidi katika eneo hilo," wizara hiyo ilisema.
Ushirikiano wa kiulinzi na misheni ya Kosovo
Msemaji huyo, aliongeza kuwa jeshi la Uturuki linaendelea kuimarisha amani ya kikanda ya kikanda na kiulimwengu kupitia mafunzo na nchi washirika.
Kulingana na msemaji huyo, kutakuwa na mkutano kati ya majeshi ya majini ya Uturuki na Albania kuanzia Novemba 2 hadi 5.
Aliongeza kuwa, Uturuki inaongoza kamandi saidizi ya vikosi vya NATO huko Kosovo, kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Mazoezi ya pamoja na Misri
Kulingana na Akturk, mazoezi ya kitaifa na kimataifa yanaendelea kwa lengo la kuimarisha ufanisi wa Majeshi ya Ulinzi ya Uturuki.
Mifumo mipya yaanza kazi
Akturk aliongeza kuwa, kamandi ya jeshi la nchi kavu imemaliza ukaguzi na uthibitishaji wa vifaa vipya wa boti za Hull na Kablolu Kamikaze-2.
Kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya kijeshi ya MKE, pia imewasilisha bunduki za MAM-15.

