Dollar

42,3350

0.2 %

Euro

49,1712

0.05 %

Gram Gold

5.547,4900

-0.07 %

Quarter Gold

9.430,0100

0 %

Silver

69,2000

0.51 %

Umoja wa Afrika umetoa wito wa kuachiliwa “mara moja na bila masharti” kwa Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló, baada ya jeshi kuchukua mamlaka ya nchi hiyo kwa nguvu.

Umoja wa Afrika wataka Rais wa Guinea-Bissau aachiwe mara moja

Maafisa wa kijeshi walitangaza kuchukua “udhibiti kamili” wa nchi baada ya kuchukua mamlaka siku ya Jumatano.

Jenerali Horta N’Tam, mkuu wa majeshi, ametangaza kuwa ameapishwa kuongoza nchi siku ya Alhamisi, ikiwa ni mapinduzi ya nne tangu nchi hiyo ipate uhuru kutoka Ureno mwaka 1974.

Katika taarifa iliyotolewa kupiita mtandao wa kijamii wa X siku ya Alhamisi, Mwenyekiti wa Tume ya AU, Mahmoud Ali Youssouf, alitoa wito wa “kwa kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa Rais Embaló na maafisa wote waliokamatwa,” akisisitiza umuhimu wa pande zote kuonesha utulivu.

Kukamatwa kwa Embaló

Embaló alikamatwa Jumatano na anashikiliwa katika makao makuu ya jeshi, ambako anadaiwa “kuangaliwa vizuri,” kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi.

Afisa mkuu aliongeza kuwa Mkuu wa Itifaki na Uratibu wa Ofisi na Waziri wa Mambo ya Ndani pia wamekamatwa.

Kiongozi wa upinzani, Domingos Simões Pereira, ambaye alizuiwa na Mahakama ya Juu kushiriki katika uchaguzi wa urais wa wikendi iliyopita, pia alikamatwa Jumatano, kwa mujibu wa vyanzo viwili vilivyo karibu naye.

AU “inashutumu vikali” mapinduzi hayo, taarifa iliongeza, na kusisitiza “umuhimu wa kuheshimu mchakato unaoendelea wa uchaguzi.”

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#