Dollar

42,3350

0.2 %

Euro

49,1712

0.05 %

Gram Gold

5.547,4900

-0.07 %

Quarter Gold

9.430,0100

0 %

Silver

69,2000

0.51 %

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameishutumu serikali ya Congo kwa kuchelewesha kutia saini makubaliano ya amani yenye lengo la kumaliza mzozo katika eneo lenye utajiri wa madini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Rais Kagame aishutumu DRC kwa kuchelewesha makubaliano ya amani ya Washington

Eneo hilo limekumbwa na miongo mitatu ya vita vya silaha, vinavyogharimu mamia ya maelfu ya maisha.

Ghasia ziliongezeka mwezi Januari wakati waasi wa M23 walipoteka maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na miji ya Goma na Bukavu.

Mwezi Juni, DRC ilifikia makubaliano ya amani na Rwanda, yaliyosimamiwa na Washington, na mwezi uliofuata ilitia saini azimio la msingi ya makubaliano na M23 huko Doha kwa ajili ya "usitishaji wa kudumu wa mapigano."

Kagame asema sio Rwanda inayochelewesha makubaliano ya amani

"Kinachochelewesha, naweza kukuhakikishia... hakitoki wala haihusiani na Rwanda," Kagame alisema katika mkutano wake mrefu na waandishi wa habari.

DRC "iliweka masharti tofauti na yale ambayo yalifanywa na kukubaliwa huko Washington, Marekani", Rais Kagama alidai.

"Kwa hiyo hiki ndicho kinachochelewesha mambo."

Ofisi ya rais wa DRC imeiambia shirika la AFP kwamba makubaliano ya amani yanaweza kutiwa saini mjini Washington tarehe 4 Disemba kati ya Kagame na mwenzake wa Congo Felix Tshisekedi, ingawa hakuna kilichothibitishwa.

Kuongeza juhudi

"Sina hakika kwamba tutakutana Washington" mapema Desemba, Kagame alisema.

"Tutasubiri na kuendelea kutumaini."

Mwezi Novemba, nchi hizo mbili zilikiri kutokuwepo kwa maendeleo na kuahidi "kuongeza maradufu juhudi zao za kutekeleza makubaliano ya amani ya Washington", kulingana na taarifa ya pamoja iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#