Dollar

42,3350

0.2 %

Euro

49,1712

0.05 %

Gram Gold

5.547,4900

-0.07 %

Quarter Gold

9.430,0100

0 %

Silver

69,2000

0.51 %

Kamanda wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, ambaye anapigana dhidi ya kikosi hasimu cha wapiganaji wa RSF tangu Aprili 2023, amemwomba Rais wa Marekani, Donald Trump, kusaidia kuleta amani.

Kiongozi wa jeshi la Sudan atoa wito kwa Trump asaidie kusitisha vita nchini humo

“Watu wa Sudan sasa wanangoja Washington ichukue hatua inayofuata: kuchangia katika ukweli na kazi ya Rais wa Marekani na kushirikiana nasi—na wale wa eneo hili wanaotafuta amani kwa dhati, kuumaliza huu mgogoro,” aliandika kiongozi huyo wa serikali katika makala yake iliyochapishwa kwenye The Wall Street Journal.

Jitihada za kuleta amani kati ya Burhan na aliyekuwa naibu wake, kamanda wa wapiganaji wa RSF, Mohamed Hamdan Dagalo, hazikufua dafu, huku vita hiyvo vikisababisha mauaji ya maelfu ya watu, kuwalazimisha watu milioni 12 kuhama makazi yao, na kusababisha mizozo mikubwa zaidi ya njaa na uhamishaji duniani.

Trump alionyesha nia ya kushughulikia vita hivyo kwa mara ya kwanza wiki iliyopita, akiahidi angevimaliza baada ya Mwana Mfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia kumtaka aingilie kati.

Sitisho la mapigano

“Kile ambacho Wasudan wengi wanaamini ni kwamba Bwana Trump ni kiongozi anayezungumza moja kwa moja na kuchukua hatua kwa uthabiti. Wengi wanaamini ana ujasiri wa kukabiliana na wahusika wa kigeni wanaoendeleza mateso yetu,” aliandika Burhan.

Hata hivyo, hakulitaja moja kwa moja taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), ingawa mara nyingi amelilaumu kuwasaidia wapiganaji wa RSF, madai ambayo UAE imeyakanusha mara zote.

Marekani na UAE, pamoja na Saudi Arabia na Misri, kwa sasa wanajaribu kusimamia mazungumzo ya kusitisha vita.

Katika makala yake ya maneno 1,200 iliyochapishwa Jumatano, Burhan alisema uchaguzi uliopo ni “kati ya taifa huru linalojaribu kuwalinda raia wake na kundi la wapiganaji linalotekeleza mauaji ya halaiki na kujizatiti kuangamiza jamii.”

Mapambano ya kupigania madaraka

Burhan, ambaye ni mwanajeshi wa muda mrefu, aliandika Jumatano kuwa: “Nilitambua mapema kwamba RSF ilikuwa bomu linalosubiri kulipuka.”

Kamanda wa RSF, Dagalo, ambaye wapiganaji wake awali waliandikishwa na serikali ya Khartoum kupigana kwenye maeneo ya pembezoni mwa nchi hiyo alikuwa msaidizi wa Burhan baada ya vuguvugu la wananchi la 2018–2019.

Mgogoro wa madaraka ukazuka na kugeuka vita mnamo Aprili 2023.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#