Sport
Dollar
42,3350
0.2 %Euro
49,1712
0.05 %Gram Gold
5.547,4900
-0.07 %Quarter Gold
9.430,0100
0 %Silver
69,2000
0.51 %Honorine Porsche kwanza alikiri kuchukuwa pesa lakini baadaye akadai kuwa aliibiwa na maafisa wa usalama walioingia kwenye benki hiyo.
Mwanamke raia wa Ujerumani mwenye asili ya Congo alifungwa miaka 10 jela siku ya Jumatano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa jaribio la wizi wa benki.
Honorine Porsche, 37, alifikishwa katika mahakama ya kijeshi mji mkuu wa DRC, Kinshasa, akionekana amechoka alipopatikana na hatia ya wizi wa mabavu.
Oktoba 17, karibu saa sita mchana, tawi la RawBank mjini Kinshasa lilizungukwa na maafisa wa usalama baada ya kulengwa katika shambulio.
Vurugu zikazuka ambazo ziliendelea kwa saa kadhaa, kabla ya watu watano, akiwemo Porsche, kukamatwa ndani ya benki hiyo. Hakuna aliyejeruhiwa kwenye tukio hilo.
Kulingana na benki hiyo, fedha kiasi sawa na dola $20,000 taslimu zilipotea na hazijapatikana bado.
Wakati wa kesi hiyo, Porsche kwanza alikiri kuchukuwa pesa lakini baadaye akadai kuwa aliibiwa na maafisa wa usalama walioingia kwenye benki hiyo.
Hasira mitandaoni
Kufuatia kukamatwa kwake, mwanamke huyo Mjerumani alionekana akiwa amevaa nguo sehemu moja katika video zilizosambazwa mitandaoni, huku maafisa wa usalama wakionekana kumtomasatomasa na kumnyanyasa kingono. Video hizo zilizua hasira nchini DRC.
Porsche alikataa kuzungumza mahakamani siku ya Jumatano, akiliambia shirika la AFP wakati akiondoka mahakamani kuwa "hakuwa na nguvu a kuzungumza".
Keno Grade, Balozi mdogo wa Ujerumani mjini Kinshasa, ambaye alikuwepo mahakamani, hakuzungumzia lolote kuhusu hilo.
Wakili wa Porsche anasema kuwa atakata rufaa.
Comments
No comments Yet
Comment