Sport
Dollar
42,3350
0.2 %Euro
49,1712
0.05 %Gram Gold
5.547,4900
-0.07 %Quarter Gold
9.430,0100
0 %Silver
69,2000
0.51 %Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, ametangaza hali ya dharura ya usalama nchini kote kufuatia msururu wa mauaji na utekaji wa watu.
Rais Bola Tinubu, katika taarifa iliyotolewa kutoka Ikulu na kuchapishwa kupitia mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) siku ya Jumatano, ameagiza idara ya polisi kuajiri askari wapya 20,000 ili kukabiliana na ukosefu wa usalama, na kufanya idadi ya askari wanaopangwa kuajiriwa kufikia 50,000. Hapo awali ametoa maagizo ya kuajiri askari 30,000.
“Ingawa awali nilikuwa nimeidhinisha upanuzi wa kitaifa wa vituo vya mafunzo ya polisi, mamlaka ya polisi kwa taarifa hii imepewa ruhusa kutumia kambi mbalimbali za Shirika la Huduma ya Vijana (NYSC) kama vituo vya mafunzo,” alisema.
“Askari watakaotolewa kwenye majukumu ya ulinzi wa Viongozi Wakuu (VIP) wanapaswa kupatiwa mafunzo ya dharura ili wapate maarifa na kutoa huduma bora za polisi wakati wanapopelekwa katika maeneo yenye changamoto za usalama.”
‘Kuongeza idadi ya askari mitaani’
Rais pia ameagiza Idara ya Hudumu za Serikali, kuwatuma walinzi wa misitu waliofunzwa kuwasaka magaidi misituni.
“Wanaigeria wenzangu, hii ni dharura ya kitaifa, na tunajibu kwa kupeleka askari zaidi mitaani, hasa katika maeneo yenye changamoto za usalama. Nyakati hizi zinahitaji sote tushirikiane. Kama Wanaigeria, sote tunapaswa kushirikiana katika kuhakikisha usalama wa taifa letu,” alisema Tinubu.
Rais aliiita Bunge la Kitaifa kupitisha marekebisho ya sheria ili kuruhusu mikoa kuanzisha polisi wa mkoa pale inapohitajika, na pia kuhimiza mamlaka za mitaa na taasisi za kidini kuboresha hatua za usalama.
Aliiomba jamii ya Nigeria kutoogopa, akisisitiza kuwa serikali inaendelea kujitolea kulinda raia, kuhakikisha mshikamano wa kitaifa, na kusaidia vikosi vya usalama kurejesha amani.
‘Tuko pamoja katika mapambano haya’
“Taarifu kuhusu shughuli zisizo za kawaida. Shirikiana na vyombo vya usalama. Tuko pamoja katika mapambano haya, na pamoja tutashinda,” alisema.
Wiki iliyopita, watoto zaidi ya 300 wa shule walitekwa nyara kutoka shule ya Kikristo nchini jimbo la Niger, kaskazini-mashariki mwa nchi.
Mapema mwezi huu, Rais wa Marekani, Donald Trump, alitishia Nigeria hatua za kijeshi kwa madai ya mauaji ya Wakristo. Abuja imekataa madai hayo, ikisema ni madai yasio na uhalisia.
Comments
No comments Yet
Comment