Dollar

42,3350

0.2 %

Euro

49,1712

0.05 %

Gram Gold

5.547,4900

-0.07 %

Quarter Gold

9.430,0100

0 %

Silver

69,2000

0.51 %

Maafisa, wanaojiita “Kamandi Kuu ya Kijeshi kwa Urejeshaji wa Usalama wa Kitaifa na Utulivu wa Umma,” wamechukua madaraka katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Kiongozi wa mapinduzi Guinea-Bissau, atangazwa kuwa 'Rais wa mpito’

Jenerali Horta Inta-A ametangazwa kuwa “Rais wa mpito” nchini Guinea-Bissau siku ya Alhamisi kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa Rais Umaro Sissoco Embalo madarakani, kulingana na kituo cha utangazaji cha taifa cha nchi hiyo, TGB.

Katika taarifa iliyotangazwa kwenye televisheni ya taifa siku ya Jumatano, kundi la maafisa wa jeshi waliojitambulisha kama “Kamandi Kuu ya Kijeshi kwa Urejeshaji wa Usalama wa Kitaifa na Utulivu wa Umma” lilitangaza kuwa limechukua “mamlaka yote ya dola.”

Jeshi lilisitisha shughuli zote za vyombo vya habari, likasimamisha mchakato unaoendelea wa uchaguzi, kufunga mipaka yote, na kuweka amri ya kutotoka nje ya saa tisa kuanzia saa tatu usiku kwa saa za eneo (2100 GMT).

Viongozi wa ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi waliitaka Umoja wa Afrika (AU) na ECOWAS kuchukua hatua muhimu kurejesha utawala wa kikatiba katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#