Sport
Dollar
0,0000
%Euro
0,0000
%Gram Gold
0,0000
%Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Rais Trump amesema Iran imekuwa ikijaribu kuwasiliana naye mara kwa mara wakati Marekani ikipeleka nguvu za kijeshi katika eneo hilo.
Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Iran inataka kufanya makubaliano na Marekani, wakati Marekani ikipeleka nguvu za kijeshi Mashariki ya Kati, ikiwemo meli ya kivita.
Akizungumza katika mahojiano na shirika la habari la Axios siku ya Jumatatu, Trump alisema hali kuhusu Iran “inabadilika mara kwa mara,” akiashiria kuwasili kwa kile alichokiita “msafara mkubwa wa kijeshi” karibu na Iran.
“Wanataka tufikie makubaliano. Najua hilo. Wamepiga simu mara nyingi. Wanataka kuzungumza,” alisema Trump.
Marekani imepeleka meli ya kivita ya ‘USS Abraham Lincoln’ Mashariki ya Kati, huku nchi hiyo ikiimarisha uwepo wake wa kijeshi katika eneo hilo.
Meli hiyo ya kivita ya daraja la Nimitz imeingia katika eneo hilo “ili kuimarisha usalama na utulivu wa kikanda,” kwa mujibu wa Kamandi Kuu ya Kijeshi ya Marekani (CENTCOM).
Iran ilikumbwa na wimbi la maandamano mwezi uliopita, yakianza tarehe 28 Disemba katika Soko Kuu la Tehran (Grand Bazaar), kufuatia kushuka kwa thamani ya sarafu ya Iran (rial) na kuzorota kwa hali ya uchumi.
Baadaye maandamano hayo yalisambaa hadi miji mingine kadhaa.
Trump amekuwa akitishia mara kwa mara kufanya “mashambulio makali” iwapo waandamanaji wangeuawa, lakini baadaye alighairi kauli yake, akidokeza kuwa Tehran ilikuwa imefuta mamia ya hukumu za kunyongwa zilizopangwa.
Maafisa wa Iran wameituhumu Marekani na Israel kwa kuunga mkono kile walichokiita “waasi wenye silaha,” na wameonya kuwa shambulio lolote la Marekani litajibiwa kwa “haraka na kwa nguvu zote.”
Mwezi Juni uliopita, Israel, kwa kuungwa mkono na Marekani, ilianzisha vita vya siku 12 dhidi ya Iran, jambo lililosababisha Iran kujibu kwa mashambulizi ya droni na makombora, kabla ya Marekani kutangaza kusitishwa kwa mapigano.
Comments
No comments Yet
Comment