Dollar

43,3818

0.03 %

Euro

51,3809

0.15 %

Gram Gold

7.079,7700

1.93 %

Quarter Gold

11.909,7000

2.81 %

Silver

152,5400

6.69 %

Makubaliano kati ya Benki ya Dunia na Qatar pia yanajumuisha kutengenezwa kwa ajira na kusaidia nchi zilizoathiriwa na migogoro ya silaha.

Benki ya Dunia na Qatar kusaidia kusambaza umeme kwa watu milioni 300 barani Afrika

Benki ya Dunia (WBG) na Mfuko wa Maendeleo wa Qatar (QFFD) wamesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ili kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika kutoa suluhisho bunifu na endelevu za maendeleo duniani kote, ikiwemo kuongeza upatikanaji wa huduma za umeme katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Makubaliano hayo, yaliyosainiwa wakati wa ufunguzi rasmi wa ofisi ya Benki ya Dunia mjini Doha siku ya Jumapili, yanatarajiwa kusaidia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Qatar 2030 na kuimarisha ushiriki wa Benki ya Dunia na sekta za umma na binafsi za Qatar.

Ofisi hiyo pia itatumika kama jukwaa la kukuza uwekezaji wa nje kuelekea masoko yanayoibuka katika eneo hilo na duniani kwa ujumla.

Ushirikiano huu unaakisi dhamira ya pamoja ya kuendeleza ufadhili bunifu wa maendeleo, kusaidia ujenzi upya, kuimarisha uchumi, na kutengeneza ajira katika Mashariki ya Kati, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, pamoja na maeneo yaliyoathiriwa na migogoro.

Kupitia uhamasishaji wa zana za sekta ya umma na binafsi, ushirikiano huu utalenga kufungua fursa katika sekta muhimu, uthabiti, na ukuaji jumuishi, ikiwemo maendeleo ya rasilimali watu, nishati na madini, biashara ya kilimo, na maendeleo ya kidijitali.

Kuimarisha fursa za kiuchumi

Katika makubaliano ya WBG na QFFD wanakusudia kushirikiana katika kusaidia nchi zinazostahiki kupewa vipaumbele vya maendeleo ya kimataifa. Hii inajumuisha juhudi za kupanua upatikanaji wa umeme kwa watu milioni 300 katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mpango wa M-300, na kuboresha maisha ya wakulima wadogo milioni 250 duniani kupitia jukwaa la AgriConnect la Benki ya Dunia.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Fahad Hamad Al-Sulaiti, Mkurugenzi Mkuu wa QFFD, alisema: “Hatua hii muhimu inaakisi dhamira ya muda mrefu ya Taifa la Qatar ya kuimarisha ushirikiano na taasisi kuu za kimataifa za kifedha na kuharakisha utekelezaji wa programu za maendeleo endelevu, kulingana na malengo ya Dira ya Taifa ya Qatar 2030.”

Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, alisema: “Ushirikiano wetu na Mfuko wa Maendeleo wa Qatar unaoanisha vipaumbele vya kimkakati vya pamoja na uwezo wa kukakamilishana ili kuimarisha kutengenezwa kwa ajira—na kuimarisha fursa za kiuchumi katika maeneo ambako ajira ni muhimu kwa uthabiti wa muda mrefu.”

Hatua hii pia inaendelea kuimarisha nafasi ya Qatar kama kitovu cha kimataifa cha ushirikiano wa kiuchumi na kifedha, na inaangazia jukumu la QFFD kama kichocheo cha ushirikiano wa kimataifa wenye athari chanya katika kuendeleza maendeleo ya haki na endelevu.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#