Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Thamani ya dhahabu yafikia kiwango cha juu zaidi kuwahi kutokea, gramu 28.35 ya dhahabu sasa inauzwa dola 5,000 za Marekani, huku mvutano wa kisiasa wa kimataifa ukiongezeka.

Thamani ya dhahabu yapanda kwa kiwango cha juu zaidi kutokana ni migogoro ya kimatiafa

Kuongezeka kwa bei ya dhahabu kumechochewa na wasiwasi wa masoko kuhusu mwelekeo wa sera za kigeni za Marekani na hali ya kisiasa duniani kwa ujumla.

Bei ya dhahabu iliendelea kupanda kwa kasi siku ya Jumatatu, ikivuka kwa mara ya kwanza kiwango cha dola 5,000 kwa gramu 28.35 (wakia moja). Kupanda huku kumesababishwa na hali endelevu ya sintofahamu ya kisiasa na kiuchumi duniani, hali inayowasukuma wawekezaji kukimbilia kununua dhahabu.

Bei ya dhahabu ya kuuza na kununua papo kwa hapo (spot gold) ilipanda kwa takribani asilimia 2.2 hadi kufikia dola 5,090.8 kwa wakia moja kufikia saa nne za asubuhi (07:00 GMT,) baada ya kufikia rekodi ya juu kabisa ya dola 5,111.11. Kwa ujumla, bei ya dhahabu imeongezeka kwa karibu asilimia 9.1 ndani ya wiki moja.

Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, bei ya dhahabu imepanda kwa takribani asilimia 84, na kwa karibu asilimia 17 tangu mwanzo wa mwaka huu. Kupanda huku kumechangiwa na kuongezeka kwa migogoro ya kibiashara na kisiasa duniani, pamoja na benki kuu kubwa kupunguza viwango vya riba.

Fedha (silver) nayo haikubaki nyuma; bei yake ilipanda kwa asilimia 4.6 hadi dola 107.6 kwa wakia moja, baada ya kufikia kiwango cha juu kabisa cha dola 109.46. Kwa mwaka mmoja uliopita, bei ya fedha imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 252.

Vitisho vya Trump

Washiriki wa soko walisema kuwa hofu mpya za kisiasa zimekuwa chanzo kikuu cha kupanda kwa bei, ikiwemo vitisho vya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusiana na eneo la Greenland.

Zaidi ya hayo, kauli za Trump kuhusu hali ya Iran ziliongeza wasiwasi na kutokuwa na uhakika katika masoko ya kimataifa.

Pia, siku ya Jumamosi Trump alitishia kutoza ushuru wa asilimia 100 kwa bidhaa zote za Canada zinazoingia Marekani iwapo Ottawa itafanya makubaliano ya kibiashara na China.

“Iwapo Canada itafanya makubaliano na China, itatozwa mara moja ushuru wa asilimia 100 kwa bidhaa zote za Canada zinazoingia Marekani,” Trump aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#