Dollar

43,3725

0.25 %

Euro

51,3279

0.73 %

Gram Gold

6.945,5100

1.57 %

Quarter Gold

11.455,2500

2.32 %

Silver

142,9700

6.92 %

Kitita cha huduma muhimu kwa awamu ya kwanza kitaanza kutumika Januari 26, 2026, kwa kundi la wananchi watakaogharamiwa na serikali, kulingana na Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Mohamed Mchengerwa.

Tanzania: Utekelezwaji wa Bima ya Afya kwa Wote kuanza Januari 26

Serikali ya Tanzania imetangaza kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya Bima ya Afya kwa Wote (BAW), hatua inayolenga kuwaondolea mzigo wa gharama za matibabu wananchi wasio na uwezo wakiwemo wazee, watoto, wajawazito na watu wenye ulemavu, ambao gharama zao zitabebwa na serikali.

Kulingana na Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Mohamed Mchengerwa, kitita cha cha huduma muhimu kwa awamu ya kwanza kitaanza kutumika Januari 26, 2026, kwa kundi la wananchi watakaogharamiwa na serikali.

Akizungumza jijini Dodoma Januari 24, 2026 wakati wa wakati wa kikao kazi cha kitaifa cha kujadili utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, Mchengerwa alisema kuwa awamu ya kwanza ya utekelezaji itaambatana na kuanza kutumika kwa Kitita cha Huduma Muhimu, kitakachotolewa na skimu za Bima ya Afya wakilenga makundi yaliyo hatarini ili kupata huduma za afya bila kikwazo cha fedha.

"Bei ya kitita hicho ni Sh150,000 (Dola 58) kwa kaya isiyozidi watu sita, kikiwa kinazingatia utaratibu wa rufaa katika vituo vya afya vilivyoingia mkataba na Skimu za Bima ya Afya," alisema.

Kulingana na Mchengerwa, Bima ya Afya kwa Wote si mradi wa Wizara moja bali ni ahadi ya Taifa kwa wananchi wake, mafanikio ya mpango huo yatapimwa si kwa hotuba wala maagizo, bali kwa idadi ya wananchi wanaolindwa dhidi ya gharama za matibabu na wanaopata huduma kwa heshima.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#