Dollar

43,3717

0.25 %

Euro

50,9411

0.02 %

Gram Gold

6.846,2700

0.12 %

Quarter Gold

11.353,8700

1.42 %

Silver

136,6200

2.17 %

Ziara yake ya Afrika imehusisha matukio ya kipekee kama kushindana mbio na duma nchini Afrika Kusini, kucheza mechi ya soka na watoto 100 nchini Angola, kutembelea jamii ya Wamaasai nchini Kenya, pamoja na kuhudhuria fainali ya AFCON nchini Morocco.

Nyota wa YouTube IShowSpeed afikisha wafuasi milioni 50 akiwa Afrika

Nyota wa YouTube na Twitch, IShowSpeed, amefikisha wafuasi milioni 50 kwenye mtandao wa YouTube akiwa katika ziara yake barani Afrika.

Mtengeneza maudhui huyo kutoka Marekani alitembelea jiji la Lagos, Nigeria—kitovu cha utamaduni na uchumi wa nchi hiyo—siku ya Jumatano kama sehemu ya ziara yake ya Afrika. Akiwa Lagos, aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kusherehekea kufikisha wafuasi milioni 50 kwenye YouTube.

Ziara ya IShowSpeed ilianza tarehe 29 Disemba, ambapo amesafiri katika takribani nchi 15 barani Afrika, na katika kila nchi amevutia umati mkubwa wa mashabiki. Jarida la Rolling Stone limemtaja kuwa MtengenezajiMaudhui Mwenye Ushawishi Mkubwa Zaidi wa mwaka 2025, huku jarida la Forbes likikadiria utajiri wake kufikia dola milioni 20 za Kimarekani.

Akiwa Lagos, IShowSpeed alianza ziara yake katika soko lenye shughuli nyingi la Balogun lililopo Lagos Island, ambako alikumbana na umati wa watu waliomzomea na kumuomba pesa. Akiwa amezungukwa na walinzi, alishangaa akisema: “Wanasema nini? Ni kama wanazungumza Kiingereza, lakini aina tofauti ya Kiingereza,” kabla ya kuondoka haraka sokoni humo.

Katika Freedom Park, eneo lililojengwa mahali palipokuwa gereza la zamani, alionja kwa mara ya kwanza wali wa jollof na kushangazwa na ukali wa pilipili yake. Baadaye alitembelea Nike Art Gallery, eneo maarufu linalotembelewa na watu mashuhuri na viongozi wa kisiasa wanaofika Lagos.

“IShowSpeed anaonesha utamaduni, mahusiano, tofauti za kitamaduni na chakula,” alisema Stephen Oluwafisayomi, mtengeneza maudhui mwenye umri wa miaka 24 anayefahamika kama Stevosky, alipokuwa Freedom Park. “Anataka Wamarekani waione Afrika kama mahali wanapoweza pia kuja,” aliongeza.

Mnamo saa kumi na mbili jioni (17 GMT), akiwa anaendelea kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, IShowSpeed alisimamisha msafara wake wa ulinzi pembeni ya barabara ili kushuhudia chaneli yake katika mtandao wa YouTube ikifikisha wanachama milioni 50.

“Huenda akawa ameonesha changamoto zinazokabili baadhi ya nchi, lakini hio inaweza kuwahamasisha watu kusaidia, kuchangia na kujitahidi kuboresha hali hizo, iwe kwa kuanzisha biashara, kukusanya misaada au njia nyingine,” alisema Karim Jari, mwanafunzi wa shule ya sekondari mwenye umri wa miaka 18 aliyekutwa katika Nike Art Gallery.

Siku moja kabla, IShowSpeed alishiriki sherehe za ushindi wa Senegal katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mjini Dakar.

Mzaliwa wa Cincinnati kwa jina halisi Darren Jason Watkins Jr., IShowSpeed alianza kupata umaarufu takribani miaka 10 iliyopita, akianza na maudhui ya michezo ya video kabla ya kupanua wigo wake na kuanza kushiriki safari zake mbalimbali duniani.

Ziara yake ya Afrika imehusisha matukio ya kipekee kama kushindana mbio na duma nchini Afrika Kusini, kucheza mechi ya soka na watoto 100 nchini Angola, kutembelea jamii ya Wamaasai nchini Kenya, pamoja na kuhudhuria fainali ya AFCON nchini Morocco.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#