Sport
Dollar
43,3717
0.25 %Euro
50,9411
0.02 %Gram Gold
6.846,2700
0.12 %Quarter Gold
11.353,8700
1.42 %Silver
136,6200
2.17 %Akizungumzia tishio kutoka kwa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo na mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba, Wine alisema:“Mimi si mhalifu bali mgombea Urais na sio hatia kugombea dhidi ya baba yake.”
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, amesema kuwa yeye si mhalifu, baada ya kukimbilia mafichoni kufuatia matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa wiki iliyopita nchini humo.
Wine, mwenye umri wa miaka 43, anadaiwa kukimbilia kusikojukulikana, baada ya makazi yake kuvamiwa.
Wine, ambaye aliuita uchaguzi wa Alhamisi iliyopita kama “wizi wa waziwazi”, amesema kuwa ameendelea kuwa mafichoni, akiwa ulinzi na watu wa ‘kawaida sana’.
Akizungumzia tishio kutoka kwa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo na mtoto wa Rais Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba, Wine alisema:
“Mimi si mhalifu bali mgombea Urais na sio hatia kugombea dhidi ya baba yake.”
Siku ya Jumanne, Kainerugaba, alionesha matamanio yake ya kumrithi baba yake, akiweka wazi azma yake ya kuuondoa uhai wa Wine, kupitia ukurasa wa X.
"Tumeua magaidi 22 wa NUP toka wiki iliyopita,” aliandika Kainerugaba.
"Ninaomba wa 23 awe Kabobi.”
Comments
No comments Yet
Comment