Dollar

0,0000

%

Euro

0,0000

%

Gram Gold

0,0000

%

Quarter Gold

0,0000

%

Silver

0,0000

%

Rais wa Marekani Donald Trump alisema siku ya Jumatano kwamba anaamini makubaliano yanaweze kupatikana kati ya Misri na Ethiopia, akiashiria juhudi za kutatua mzozo wao wa muda mrefu kuhusu Bwawa kubwa lililojengwa na Ethiopia.

Trump anasema makubaliano yanaweza kupatikana kati ya Misri na Ethiopia kuhusu mzozo wa bwawa

Rais wa Marekani Donald Trump alisema bwawa hilo "kimsingi linazuia Mto Nile," akipendekeza kwamba "ataona kama naweza kufanikisha makubaliano kati ya nchi hizo mbili.

"Ni jambo la hatari. Walijenga bwawa ambalo linazuia watu fulani kupata maji ambayo wanastahili kuapata na ambayo wamekuwa wakipata kwa miaka milioni moja, na ghafla mtiririko wa maji unazibwa na bwawa kubwa sana," Trump alisema, katika mkutano wake na Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi nchini Marekani.

"Nadhani tutaweza kupata masikizano kuhusu bwawa. Bwawa ni tatizo kubwa. Tutaweza kufanya kitu," aliongeza.

Uzinduzi wa bwawa

Wiki iliyopita, Trump alijitolea kufanya upatanishi kati ya Misri na Ethiopia, huku Sisi akiipongeza hatua hiyo ya Trump.

Mto Nile, ambao una urefu wa kilomita 6,650, unashirikiwa na nchi 11: Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Uganda, Tanzania, Ethiopia, Eritrea, Sudan Kusini, Sudan na Misri.

Serikali ya Ethiopia ilizindua Bwawa la Ethiopia kwenye Mto Nile mnamo Septemba 9, 2025, baada ya miaka 14 ya ujenzi, mradi ambao umekuwa ukipingwa kwa muda mrefu na nchi ya Misri na Sudan.

Misri na Sudan kwa muda mrefu zimeitaka Ethiopia kufikia makubaliano ya kisheria ya pande tatu kuhusu kujaza na kuendeshwa kwa bwawa hilo.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#