Sport
Dollar
43,3725
0.25 %Euro
51,3279
0.73 %Gram Gold
6.945,5100
1.57 %Quarter Gold
11.455,2500
2.32 %Silver
142,9700
6.92 %Nchini Rwanda, muhudumu mmoja wa afya huhudumia wagonjwa 1,000, ambao ni uwiano tofauti na ule pendekezwa wa wahudumu wa afya wanne kwa kila wagonjwa 1,000.
Rwanda itafanya majaribio ya teknolojia ya Akili Mnemba (AI) kwenye kliniki zaiid ya 50, ikiwa ni sehemu ya mradi wa taasisi ya Gates, unaolenga kuboresha huduma za afya barani Afrika.
Teknolojia hiyo, inalenga utoaji huduma za kliniki hiki pamoja na kuongeza ufanisi, kulingana na Andrew Muhire, afisa afya kutoka Wizara ya Afya nchini humo.
Nchini Rwanda, muhudumu mmoja wa afya huhudumia wagonjwa 1,000, ambao ni uwiano tofauti na ule pendekezwa wa wahudumu wa afya wanne kwa kila wagonjwa 1,000.
Siku ya Jumatano, taasisi ya Gates na OpenAI, zilizindua mkakati mpya ujulikanao kama Horizons1000, wenye thamani ya Dola Milioni 50, ndani ya kipindi cha miaka miwili.
Kulingana na Bill Gates, mradi huo unalenga kupunguza pengo la kukosekana usawa katika utoaji huduma za afya.
“Akili Mnemba ndilo suluhisho pekee katika kuboresha miundombinu kwenye sekta ya afya,” alisema Gates.
Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya kidijiti wana wasiwasi matumizi ya Akili Mnemba kwa lugha ya Kiingereza, itagandamiza lugha zingine za nchini Rwanda.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa AI na kampuni ya kidijiti ya Umuganda, Audace Niyonkuru amesema kuna jitihada za kuiweka lugha ya Kinyarwanda kwenye mfumo huo.
Lugha hiyo huzungumzwa na asilima 75 ya raia wa Rwanda.
Comments
No comments Yet
Comment