Sport
Dollar
43,3679
0.25 %Euro
51,1360
0.4 %Gram Gold
6.951,6600
1.66 %Quarter Gold
11.455,2500
2.32 %Silver
140,5100
5.08 %Rais wa Uganda Yoweri Museveni, mwenye umri wa miaka 81, alishinda muhula wake wa saba kwa kupata asilimia 72 ya kura dhidi ya mpinzani wake Bobi Wine ambaye amepata asilimia 25, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi nchini Uganda.
Mkuu wa majeshi nchini Uganda ambaye pia ni mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugana amesema siku ya Ijumaa kuwa wanachama 30 wa upinzani wameuawa na watu 2,000 kukamatwa baada ya uchaguzi.
“Tumewakamata zaidi ya wahuni 2,000 ambao Kabobi alidhani angewatumia,” aliandika mkuu wa majeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba kwenye mtandao wa X, akitumia jina la kumkejeli Bobi Wine (Kabobi).
“Mpaka sasa tumewaua magaidi 30 wa NUP,” alisema, akiashiria chama cha Bobi Wine, cha National Unity Platform (NUP).
Kiongozi wa upinzani Bobi Wine bado yuko mafichoni baada ya kushtumu vikosi vya usalama kwa kuvamia nyumba yake kufuatia uchaguzi uliofanyika Januari 15.
Ameutaja uchaguzi huo kama “wizi wa waziwazi” na kutoa wito kwa wananchi kuandamana.
Rais Museveni, 81, alishinda muhula wake wa saba kwa kupata asilimia 72 ya kura dhidi ya mpinzani wake Bobi Wine ambaye amepata asilimia 25, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi nchini Uganda.
Rais Yoweri Museveni aliwaambia wananchi Jumapili kwamba ushindi wake mkubwa katika uchaguzi wa Uganda unaonyesha “umaarufu yn nguvu” ya chama chake cha National Resistance Movement (NRM).
Miongoni mwa waliokamatwa katika siku za hivi karibuni ni mbunge wa upinzani Muwanga Kivumbi kutoka eneo la Butambala katikati mwa Uganda, ambako vurugu kubwa zaidi za siku ya uchaguzi ziliripotiwa.
Kivumbi aliiambia shirika la habari la AFP kwamba vikosi vya usalama viliwaua wanachama wake 10 wa kampeni baada ya kuvamia nyumba yake, huku polisi wakisema kuwa wafuasi wake walipigwa risasi walipokuwa wakijaribu kuchoma kituo cha kuhesabia kura na kituo cha polisi.
Comments
No comments Yet
Comment