Sport
Dollar
43,3613
0.23 %Euro
50,9496
0.04 %Gram Gold
6.894,3100
0.83 %Quarter Gold
11.461,4600
2.38 %Silver
138,5600
3.63 %Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco alisema siku ya Alhamisi kuwa undugu wa Afrika utaendelea kushamiri licha ya kile alichokiita vitendo “vya kusikitisha” vilivyotia doa fainali ya AFCON dakika za mwisho kati ya Morocco na Senegal.
Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco alisema kuwa, “Hakuna kitu kinachoweza kutatiza uhusiano wa karibu uliojengwa kwa karne nyingi miongoni mwa watu wa Afrika, wala ushirikiano wenye manufaa uliojengwa kote barani na kuimarishwa kupitia ushirikiano wenye malengo makubwa zaidi.”
Haya yanajiri baada ya wachezaji wa Senegal kuondoka uwanjani wakipinga penati iliyotolewa kwa Morocco dakika za mwisho za mchezo, kabla ya kurejea na kuifunga Morocco 1–0 katika kipindi cha muda wa ziada siku ya Jumapili.
Hali hii ilisababisha mtafaruku na vurugu kati ya mashabiki wa timu hizo mbili.
Kwa muda mrefu, Senegal imekuwa miongoni mwa washirika wa karibu zaidi wa Morocco barani Afrika, ambapo kampuni na benki za Morocco zimepanua uwekezaji wao katika miaka ya hivi karibuni, jambo lililoimarisha ushawishi wa kidiplomasia wa mfalme huyo.
Masaa machache baada ya fainali, mitandao ya kijamii katika nchi zote mbili ilishuhudia hali ya mvutano kila pande ikitoa hisia kali kufuatia yaliyojiri katika fainali hiyo.
Alisema pia kuwa mashindano hayo yalionesha maendeleo ya Morocco na yaliwakilisha “mafankio kwa Afrika nzima.”
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) lilisema litachukua “hatua stahiki” baada ya kupitia matukio ya mechi hiyo, huku Rais wa FIFA, Gianni Infantino, akilaani tabia ya wachezaji wa Senegal na baadhi ya wajumbe wa benchi la ufundi.
Comments
No comments Yet
Comment