Dollar

43,3613

0.23 %

Euro

50,9496

0.04 %

Gram Gold

6.887,7400

0.73 %

Quarter Gold

11.461,4600

2.38 %

Silver

138,5100

3.59 %

Rais wa Uturuki Erdogan asema kupunguzwa kwa uhasama na utulivu wa kikanda bado ni jambo muhimu huku maandamano yakiendelea kote Iran.

Erdogan amesema Uturuki inapinga uingiliaji wa nje nchini Iran katika mazungumzo na Pezeshkian

Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan alimwambia mwenzake wa Irani Masoud Pezeshkian kupitia njia ya simu siku ya Alhamisi kwamba Uturuki inapinga uingiliaji wowote wa nje nchini Iran na kwamba inathamini amani na utulivu wa majirani zake, Ofisi ya Rais wa Uturuki iliandika kupitia mtandao wa kijamii wa X.

Katika taarifa hiyo, ofisi ya rais imesema kuwa kiongozi huyo amejadili kuhusu matukio ya hivi punde nchini Iran. Aidha, Erdogan pia alisema kutatuliwa kwa matatizo kwa njia ya utulivu kunanufaisha Uturuki.

Iran inakabiliana na maandamano makubwa zaidi dhidi ya serikali katika historia yake, uliosababisha serikali kukabiliano nao, aidha Kiongozi Mkuu Ali Khamenei alisema siku ya Jumamosi maandamano hayo ulisababisha vifo vya "maelfu kadhaa".

Ilikuwa ni mara ya kwanza kiongozi huo kukiri hadharani juu ya ukubwa wa majeruhi, ambayo aliilaumu Marekani kuyasababisha.

Maandamano na migomo ambayo awali ilichochewa na malalamiko ya kuhusu changamoto za kiuchumi iligeuka na kuwa vuguvugu kubwa dhidi ya uongozi wa ambao umeitawala Iran tangu mapinduzi ya 1979, huku watu wenfi wakimiminika kuandamana mitaani kwa siku kadhaa kuanzia tarehe 8 Januari.

Siku ya Jumatano, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alitoa onyo la moja kwa moja hadi sasa kwa Washington, akisema Jamhuri ya Kiislamu "itarudisha nyuma kila kitu tulicho nacho ikiwa tutashambuliwa upya."

Idadi rasmi ya kwanza kutoka kwa mamlaka, ilioripotiwa na televisheni ya serikali, ilisema siku ya Jumatano kwamba jumla ya watu 3,117 waliuawa wakati wa maandamano.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#