Dollar

43,3717

0.25 %

Euro

50,9411

0.02 %

Gram Gold

6.848,5000

0.16 %

Quarter Gold

11.360,9900

1.48 %

Silver

136,6900

2.23 %

Hatua hiyo inalenga kulinda meli za Uturuki, kuimarisha mapambano dhidi ya uharamia, na usalama wa baharini.

Uturuki yaongeza muda wa vikosi vyake vya wanamaji katika Ghuba ya Aden kwa mwaka mmoja

Azimio la rais la kuongeza muda wa vikosi vya Wanamaji vya Uturuki katika Ghuba ya Aden, pwani ya Somalia, Bahari ya Arabia na maeneo yanayoyazunguka kwa mwaka mmoja kuanzia Februari 10, 2026, limechapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali.

Kuongezwa huko kwa muda kunalenga kulinda meli za kibiashara zinzopeperusha bendera ya Uturuki au zinazohusishwa na Uturuki, kuchangia juhudi za kimataifa dhidi ya uharamia, uporaji wa kutumia silaha baharini na ugaidi, kusaidia operesheni za misaada ya kibinadamu, pamoja na kuimarisha uzoefu wa kiutendaji wa jeshi la wanamaji la nchi hiyo na ushirikiano wa kimataifa.

Uturuki imekuwa ikishiriki katika operesheni za kimataifa za kupambana na uharamia tangu mwaka 2009, ikiwemo Operesheni ya NATO ya ‘Ocean Shield’ na Kikosi Kazi cha Pamoja 151 (CTF-151), ambacho kimeongozwa na Uturuki mara saba kati ya 2009 na 2025.

Azimio hilo lilibainisha kuwa kufuatia ombi la Somalia kwa mkuu wa Umoja wa Mataifa, hakuna azimio lililopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tangu 2022 la kurejesha mamlaka iliyokuwa hapo awali kuhusiana na kupambana na uharamia, wizi wa kutumia silaha na ugaidi wa baharini katika Ghuba ya Aden, maji ya ardhi ya Somalia na maeneo ya karibu.

Aidha, lilibainisha kuwa operesheni za kimataifa dhidi ya uharamia na uhalifu wa baharini zinaendelea katika maeneo yaliyo nje ya maji ya eneo la Somalia chini ya Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 1851, lililopitishwa mwaka 2008.

Katika muktadha huo, azimio hilo liliangazia kuwa muda wa Operesheni ya Umoja wa Ulaya ya Atalanta iliongezwa hadi Februari 28, 2027, kufuatia uamuzi wa Baraza la Umoja wa Ulaya wa Disemba 16, 2024.

Kuongezwa muda wa operesheni hiyo ni sehemu ya wajibu wa kimataifa na wa Uturuki katika kudhibiti usalama wa baharini, uhuru wa meli kufanya shughuli zake bila ya kuingiliwa, na amani na utulivu wa kimataifa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Comments

Comment

Comment Your email address will not be published. Required fields are marked*

No comments Yet

#