Sport
Dollar
38,5682
0.32 %Euro
43,6907
0.3 %Gram Gold
4.004,2000
0 %Quarter Gold
0,0000
%Silver
0,0000
%Chama hicho kimeahidi kuendelea kushirikiana na taasisi zote za dini katika kujenga taifa lenye kulinda na kuendeleza misingi ya amani, umoja wa kitaifa, mshikamano, heshima na linaloheshimu haki za binadamu.
Katika taarifa yake iliyotolewa Mei 1, 2025, chama hicho tawala nchini Tanzania, kimesema kuwa kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padre Dkt. Charles Kitima.
CCM pia imetoa wito kwa vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka ili kuwabaini na kuwachukulia hatua kali wahusika wa tukio hilo.
“Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC) Padre Dkt. Charles Kitima, tukio lililotokea usiku wa Aprili 30, 2025, katika eneo la Kurasini, jijini Dar es Salaam,” imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel John Nchimbi.
Aidha, chama hicho kimetoa pole kwa Padre Dkt. Kitima na familia yake, TEC, na waumini wote wa Kanisa Katoliki kwa mshtuko na maumivu yaliyosababishwa na tukio hilo.
“Tunamuombea Padre Kitima uponaji wa haraka na kurejea katika majukumu yake ya kiroho na kijamii,” taarifa hiyo iliongeza.
Chama hicho kimeahidi kuendelea kushirikiana na taasisi zote za dini katika kujenga taifa lenye kulinda na kuendeleza misingi ya amani, umoja wa kitaifa, mshikamano, heshima na linaloheshimu haki za binadamu.
Tayari, jeshi la Polisi nchini Tanzania linamshikilia mtu mmoja aitwaye Rauli Mahabi kwa tuhuma za kumjeruhi Katibu Mkuu huyo wa TEC.
Padre Kitima alishambuliwa katika eneo la Kurasini jijini Dar es Salaam, ambako ziko ofisi za makao makuu ya TEC.
Comments
No comments Yet
Comment